Jezi Mpya ya Simba CAF 2024/2025
WAKATI kikosi cha wekundu wa Msimbazi Simba kikiwa kambini jijini Dar es Salaam kujiandaa na michezo mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika CAF, inaelezwa uongozi wa klabu hiyo umepanga kuzindua jezi mpya maalumu kwa ajili ya michuano ya kimataifa hapo kesho Jumatano, tarehe 20 Novemba 2024. Uzinduzi huu unatarajiwa kufanyika kabla ya mechi ya Simba dhidi ya Pamba Jiji, ambayo imepangwa kufanyika Novemba 22, 2024, kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza.
Ubora wa Jezi Mpya za Simba
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, jezi hizo mpya zitatambulishwa rasmi zikiwa na rangi tatu kuu: nyeupe, nyekundu, na bluu. Rangi hizi zimechaguliwa kwa umakini ili kuonyesha hadhi ya kimataifa na kushabihiana na malengo ya klabu ya kufanya vizuri katika michuano ya CAF na mashindano mengine ya kitaifa na kimataifa.
Mmoja wa maafisa wa Simba alieleza: “Tunaamini ubora wa jezi hizi kwa ajili ya mashindano makubwa ya kimataifa. Zitaanza kutumika rasmi katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.”
Jezi hizo zimebuniwa kwa kutumia teknolojia ya kisasa ili kuwapa wachezaji uhuru wa kusogea na faraja wanapokuwa uwanjani, huku zikiwa na muundo unaovutia mashabiki wa klabu hiyo maarufu nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Hizi Apa Picha za Jezi Mpya ya Simba CAF 2024/2025
Matumizi Rasmi ya Jezi
Jezi mpya za Simba zitaanza kutumika katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo Simba imepangwa kuanza dhidi ya Bravos do Maquis kutoka Angola. Mchezo huo utafanyika Novemba 27, 2024, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba ilifuzu hatua ya makundi baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya. Ushindi huo ulitokana na mchezo wa nyumbani uliochezwa jijini Dar es Salaam baada ya sare ya suluhu katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Libya.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Taifa stars Vs Guinea Leo 19/11/2024 Saa Ngapi?
- Matokeo ya Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024
- Kikosi cha Tanzania vs Guinea leo 19/11/2024
- Fadlu Davids Afurahishwa Kurejeshwa Kwa Mechi Dhidi ya Pamba Kabla ya CAFCC
- Aussems Ampa Madini Guede
- Viingilio Mechi Ya Yanga VS Yanga Vs Al Hilal 26/11/2024
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Al Hilal 26/11/2024
- Moto wa Tabora United Wawashinikiza Singida BS Kutafuta Mechi ya Kirafiki
Leave a Reply