Hizi Apa Rekodi Za Miguel Gamondi Akiwa Yanga

Rekodi za Gamondi

Hizi Apa Rekodi Za Miguel Gamondi Akiwa Yanga

Klabu ya Yanga imetangaza kuvunja mkataba wa aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi, leo Ijumaa, Novemba 15, 2024.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Yanga imesema:

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unapenda kuutarifu umma kuwa umevunja mkataba na Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza, Angel Miguel Gamondi. Vilevile, Uongozi wa Young Africans Sports Club umesitisha mkataba wa kocha msaidizi wa kikosi cha kwanza, Moussa Ndaw.

“Uongozi wa Young Africans Sports Club unawashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya. Tayari mchakato wa haraka wa kutafuta makocha wapya wa kikosi chetu umeanza.”

Miguel Gamondi ameondoka akiwa na rekodi za kipekee ambazo zitachukua muda mrefu kuvunjwa. Hapa tunakuletea kwa undani mafanikio yake na alama alizoweka akiwa na Yanga.

Hizi Apa Rekodi Za Miguel Gamondi Akiwa Yanga

Rekodi za Miguel Gamondi Akiwa Yanga

1. Mechi 40 Zenye Matokeo Mzuri

Tangu Gamondi ateuliwe kuwa kocha mkuu wa Yanga Juni 24, 2023, aliongoza jumla ya mechi 40 katika Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika mechi hizo:

  • Ushindi: 34
  • Sare: 4
  • Vipigo: 4

Katika kipindi hicho, safu ya ushambuliaji ya Yanga ilifunga mabao 85, huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara 18. Alikusanya jumla ya pointi 104 katika misimu miwili aliyokaa klabuni hapo.

2. Mataji Matatu Makubwa

Gamondi alifanikiwa kuipa Yanga mataji matatu:

  • Ligi Kuu Bara 2023/2024: Taji lililowakamilishia jumla ya mataji 30 tangu mwaka 1965.
  • Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) 2024.
  • Ngao ya Jamii 2024.

3. Kufuzu Hatua ya Makundi CAF Baada ya Miaka 25

Miguel Gamondi aliivusha Yanga katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25. Mara ya mwisho klabu hiyo kufika hatua hiyo ilikuwa mwaka 1998.

Katika msimu wa 2023/2024, Gamondi aliiwezesha Yanga kuifunga Al Merrikh ya Sudan kwa jumla ya mabao 3-0 na kufuzu kwa mbwembwe. Ushindi wa nyumbani na ugenini ulikuwa ni wa kihistoria, kwani Yanga haijawahi kushinda dhidi ya Al Merrikh hapo awali.

4. Rekodi ya Robo Fainali CAF

Chini ya Gamondi, Yanga iliandika historia kwa kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza. Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria Februari 24, 2024, uliiweka Yanga katika nafasi ya kipekee kwenye soka la Afrika.

5. Kupiku Rekodi ya Simba SC

Yanga chini ya Gamondi ilifanikiwa kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza nchini kushinda mabao mengi zaidi dhidi ya timu za Afrika Kaskazini, rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Simba. Ushindi wa 4-0 dhidi ya Belouizdad ulikuwa alama muhimu kwa Gamondi na timu yake.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kali Ongala Tambulishwa Kuwa Kocha Mpya wa KMC
  2. Ethiopia Vs Tanzania 16/11/2024 Saa Ngapi?
  3. Gamondi Akalia Kuti Kavu Yanga
  4. Kikosi cha Tanzania Vs Ethiopia 16/11/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo