Nafasi 10 Za Kazi Msaidizi Maendeleo Ya Jamii Halmashauri Ya Wilaya Ya Kyela
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela imepata kibali cha ajira mbadala kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ikiruhusu kuajiri wafanyakazi wapya. Kufuatia kibali hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela anatangaza nafasi 10 za kazi kwa ajili ya nafasi ya Msaidizi Maendeleo ya Jamii Daraja la III. Watanzania wote wenye sifa zinazostahili wanakaribishwa kutuma maombi yao.
Majukumu ya Msaidizi Maendeleo ya Jamii
Kwa mujibu wa tangazo la nafasi hizi, majukumu ya Msaidizi Maendeleo ya Jamii ni pamoja na:
- Kuratibu shughuli za maendeleo ya jamii kwa kuzingatia jinsia.
- Kuelimisha jamii katika kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathmini mipango yao ya maendeleo.
- Kuhamasisha jamii kuondokana na mila potofu na kuwa na mtazamo wa mabadiliko chanya.
- Kutoa ripoti za utekelezaji wa kazi kila mwezi.
- Kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kijinsia na umuhimu wa kujiunga na elimu ya watu wazima.
- Kuhamasisha matumizi ya teknolojia rahisi na sahihi kwa jamii.
- Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa za matukio mbalimbali kama vile vifo, magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira, na unyanyasaji wa kijinsia.
- Kukusanya na kuchambua takwimu zinazozingatia jinsia ili kuwezesha mipango bora ya maendeleo.
Msaidizi wa Maendeleo ya Jamii pia atafanya kazi zingine zozote atakazopewa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na taaluma yake.
Sifa za Mwombaji
Ili kufuzu kuomba nafasi hizi, mwombaji anapaswa kuwa na sifa zifuatazo:
- Cheti cha Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
- Cheti cha Astashahada katika Maendeleo ya Jamii au Sayansi ya Sanaa kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, Rungemba, au chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.
Masharti ya Ujumla
Masharti ya ujumla kwa waombaji ni pamoja na:
- Uraia na Umri: Mwombaji awe Raia wa Tanzania, mwenye umri wa kati ya miaka 18 na 45.
- Maombi ya Walemavu: Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanatakiwa kuainisha aina ya ulemavu walionao ili kusaidia maamuzi sahihi.
- Nyaraka Muhimu: Waombaji wote waambatanishe CV yenye taarifa binafsi kamili, majina ya wadhamini watatu wa kuaminika, na vyeti vilivyothibitishwa.
- Mafunzo na Vyeti: Waombaji waliomaliza masomo nje ya nchi wanapaswa kuhakikisha vyeti vyao vimethibitishwa na mamlaka husika (NECTA, NACTE, TCU).
- Marufuku kwa Waajiriwa wa Umma: Wale ambao tayari wako katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa wakiambatanisha kibali maalum.
- Uwasilishaji wa Taarifa Sahihi: Waombaji ambao watawasilisha taarifa au nyaraka za kughushi watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Jinsi ya Kutuma Maombi
Maombi yote ya kazi yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo wa kielektroniki wa Ajira wa Serikali (Recruitment Portal) kwa anuani ifuatayo: https://portal.ajira.go.tz. Mwombaji anatakiwa kuzingatia taratibu zote na kuambatanisha vyeti muhimu kama ilivyoelekezwa katika tangazo hili.
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela
S.L.P 320, Kyela – Mbeya
Simu: 025-2540035/7
Nukushi: 0252540425
Barua pepe: ded@kyeladc.go.tz
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 3 Novemba, 2024. Waombaji wanashauriwa kutuma maombi yao mapema ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza dakika za mwisho.
Mapendekezi ya Mhariri:
Leave a Reply