Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2024/2025 (Batch Three)

Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2024 2025 Batch Three

Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2024/2025 (Batch Three)

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu HESLB (Higher Education Students’ Loans Board)  imetangaza orodha ya wanafunzi waliopangiwa mikopo kwa Awamu ya Tatu kwa mwaka wa masomo 2024/2025. Katika awamu hii, jumla ya wanafunzi wapya 19,345 wamepata mkopo wa thamani ya TZS bilioni 59.49. Hawa ni wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanaojiunga na vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za elimu ya juu nchini Tanzania kwa ajili ya shahada ya awali katika fani mbalimbali.

Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2024/2025 (Batch Three)

Idadi ya Waliopata Mkopo kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025

Kufuatia kutangazwa kwa Awamu ya Tatu, idadi ya jumla ya wanafunzi waliopangiwa mikopo imefikia 70,990.

Thamani ya mikopo iliyotolewa hadi sasa ni TZS bilioni 223.3. Kati ya wanafunzi hawa, wanaume ni 40,164 (sawa na asilimia 56.58) na wanawake ni 30,825 (sawa na asilimia 43.42).

Mbali na mikopo kwa shahada za awali, Bodi ya Mikopo pia imepanga mikopo kwa wanafunzi wa stashahada. Katika awamu hii ya tatu, wanafunzi wapya wa stashahada 425 (ambapo 378 ni wa mwaka wa kwanza na 47 ni wanaoendelea na masomo) wamepangiwa mikopo yenye thamani ya TZS bilioni 1.1.

Mpango wa ruzuku wa ‘Samia Scholarship’ kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza pia umeendelea katika mwaka wa masomo 2024/2025. Hadi sasa, kiasi cha TZS bilioni 3.02 kimekwishatolewa kwa wanafunzi 599. Katika hawa, 588 walipokea ruzuku kwenye awamu ya kwanza na 11 walipokea kwenye awamu ya pili.

Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliopata Mkopo Awamu ya Tatu HESLB 2024/2025

Wanafunzi ambao walituma maombi ya mkopo wa elimu ya juu kupitia Dirisha la Tatu la maombi ya mkopo HESLB wanaweza kufuatilia majibu ya maombi ya mkopo HESLB kwa njia ya kupitia akaunti yao ya SIPA HESLB . Ili kuangalia kama umepata mkopo, fuata hatua hizi:

Fungua Tovuti ya HESLB: Tembelea tovuti rasmi ya HESLB au bonyeza moja kwa moja kwenye kiungo hiki https://olas.heslb.go.tz/olams/account/login.

Ingia kwenye Akaunti yako: Tumia jina la mtumiaji na nenosiri ulilojisajili nalo wakati wa kuomba mkopo.

Jinsi ya Kuangalia Mkopo HESLB 2024/2025

Mara Baada ya kuingia katika akaunti yako, Bofya Kitufe kilichoandikwa “SIPA” Kisho Bofya “ALLOCATION”

Jinsi ya Kuangalia Mkopo HESLB
jinsi ya kuangalia mkopo heslb

Chagua mwaka wa masomo. Baada ya kubofya “Allocation” Utapelekwa kwenye ukurasa mwengine ambapo unatakiwa kuchagua mwaka wa masomo (2024/2025) ili kuweza kuona kiasi cha mkopo ulicho pata.

Kuangalia kiasi cha mkopo

Angalia Taarifa zako za Mkopo: Utaweza kuona kama umepewa mkopo na kiasi kilichopangiwa. Ni muhimu kufuatilia akaunti yako mara kwa mara ili kujua hali ya maombi yako. Mabadiliko yoyote yanayohusiana na mkopo yataonekana ndani ya akaunti yako ya SIPA.

Kuangalia Majibu ya Maombi ya Mkopo HESLB

Mwongozo kwa Wanafunzi Waliofanikiwa Kupata Mkopo

Kwa wanafunzi waliopangiwa mikopo, ni muhimu kufuata hatua zinazohitajika ili kuhakikisha kwamba mikopo yao inatolewa kwa wakati na bila usumbufu. Baadhi ya hatua muhimu ni pamoja na:

  • Kuhakikisha umekamilisha usajili wako chuoni.
  • Kupeleka nakala za barua za mkopo na nyaraka nyingine zinazohitajika kwenye ofisi ya fedha ya chuo chako.
  • Kuendelea kufuatilia akaunti yako ya mkopo kupitia mfumo wa mtandao wa HESLB.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya mtihani wa Darasa La Saba
  2. Viwango Vya Mishahara Kada ya Afya 2024 (TGHS Afya Salary Scale)
  3. Vituo vya Uandikishaji Wapiga Kura Halmashauri ya Mji wa Kondoa
  4. Majina ya Waliopata Mkopo 2024/2025 HESLB
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo