Simba Vs Yanga Sc Leo 19/10/2024 Saa Ngapi?

Simba Vs Yanga Sc Leo 19 10 2024 Saa Ngapi

Simba Vs Yanga Sc Leo 19/10/2024 Saa Ngapi? 

Mchezo wa Kariakoo Dabi kati ya mahasimu wawili wakubwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC na Yanga SC, unasubiriwa kwa hamu kubwa leo Oktoba 19, 2024. Mchezo huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/2025 utachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, na utapigwa majira ya saa 11:00 jioni. Timu hizi mbili zinakutana kwa mara ya kwanza msimu huu, huku kila moja ikiwa na lengo la kuonesha ubabe wake na kuondoka na pointi tatu muhimu.

Simba Vs Yanga Sc Leo 19/10/2024 Saa Ngapi?

Historia ya Kariakoo Dabi, Mechi ya Simba Vs Yanga

Kariakoo Dabi imekuwa ni miongoni mwa michezo mikubwa na yenye mvuto zaidi ya ligi kuu Tanzania na miongoini mwa dabi kubwa barani Afrika, na kila mara inapokaribia, shauku ya mashabiki huongezeka kwa kiasi kikubwa.

Katika msimu wa 2023/24, Yanga iliibuka kidedea kwa kuifunga Simba katika michezo yote miwili ya ligi. Katika mzunguko wa kwanza, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1, na katika mzunguko wa pili Simba ilipoteza tena kwa mabao 2-1. Katika dakika zote 180 za msimu uliopita, jumla ya mabao 9 yalifungwa ambapo Yanga ilifunga mabao 7 na Simba ikapata mabao 2 pekee.

Kuelekea mechi ya leo, makocha wa timu zote mbili, Fadlu Davids wa Simba na Miguel Gamondi wa Yanga, wamekuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha timu zao zinaingia uwanjani zikiwa na maandalizi mazuri kwa ajili ya pambano hili la Kariakoo Dabi.

Maandalizi ya Simba SC

Simba SC, inayonolewa na kocha Fadlu Davids, imedhamiria kupata ushindi ili kuwaridhisha mashabiki wao baada ya matokeo yasiyoridhisha msimu uliopita dhidi ya Yanga. Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amebainisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na timu iko tayari kwa ajili ya mchezo huo muhimu. “Tuna kazi kubwa Oktoba 19, tutapambana kwa nguvu zote kuhakikisha tunapata ushindi na pointi tatu muhimu,” alisema Ahmed.

Katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/25, Simba imeanza vizuri kwa kucheza michezo mitano hadi sasa. Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Tabora United, Simba ilishinda mabao 3-0, ikifuatiwa na ushindi wa 4-0 dhidi ya Fountain Gate.

Simba pia iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC ugenini na ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji. Hata hivyo, Simba ilipata sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union katika mechi ya mwisho kabla ya Kariakoo Dabi. Simba imefunga mabao 12 hadi sasa, huku Leonel Ateba na Jean Ahoua wakiwa na mabao mawili kila mmoja.

Maandalizi ya Yanga SC

Kwa upande wa Yanga SC, benchi la ufundi linatarajia kuendeleza mwendo mzuri wa timu hiyo ambao wameuonyesha tangu mwanzo wa msimu wa 2024/25. Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, alithibitisha kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa na malengo ya kuchukua pointi tatu. “Tunajua umuhimu wa mchezo huu, na maandalizi yanaendelea kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema Kamwe.

Yanga SC imekuwa na mwanzo mzuri msimu huu ambapo haijapoteza mechi hata moja kati ya michezo minne iliyocheza hadi sasa. Katika mchezo wa kwanza, walishinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar, wakafuatiwa na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ken Gold.

Yanga pia iliwafunga KMC bao 1-0 na kupata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji. Hadi sasa, timu hiyo imeshinda mechi zote na haijaruhusu bao lolote, huku mabeki wake wakiongozwa na Ibrahim Bacca wakiwa na nidhamu nzuri ya ulinzi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Timu Zilizofuzu AFCON 2025
  2. Taifa Stars Yashushiwa Kichapo Mbele ya Maelfu Ya Mashabiki Kwa Mkapa
  3. Fred Minziro Akabidhiwa Rasmi Mikoba ya Kuinoa Pamba jiji
  4. Msimamo wa Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo