Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani Jumamosi

Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani Jumamosi

Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani

Katika maandalizi kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, beki wa kati wa Simba, Che Malone Fondoh, ametoa onyo kali kwa wachezaji wenzake, akiwataka kuwa makini zaidi na kuepuka makosa.

Mechi hiyo inayotarajiwa kuwa ya vuta nikuvute itachezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Onyo la Che Malone linakuja baada ya sare ya mabao 2-2 ambayo Simba walipata dhidi ya Coastal Union, mechi iliyowaacha mashabiki na benchi la ufundi la Simba na wasiwasi kuelekea dabi hiyo muhimu.

Che Malone amesisitiza kuwa makosa kama yale yaliyojitokeza dhidi ya Coastal Union hayapaswi kurudiwa kwenye mechi ya Jumamosi.

Amesema kuwa mechi za dabi kama hii zina uzito mkubwa, na zinaweza kuathiri mwelekeo wa msimu mzima, hasa katika harakati za kutafuta ubingwa. “Ikiwa tutarudia makosa yale yale, tunaweza kupata matokeo mabaya ambayo yatatuathiri katika mbio za ubingwa,” alisema beki huyo wa Simba, akionyesha wasiwasi wake.

Kwa upande mwingine, nyota huyo kutoka Cameroon aliongeza kuwa mechi kama hizi zinaweza kuathiri kisaikolojia wachezaji, huku baadhi ya wachezaji wakiweza kujenga majina makubwa kupitia matokeo chanya katika michezo hii.

“Mechi ya Yanga ni fainali kwetu, ni michezo ambayo inaweza kukufanya mchezaji kuwa staa zaidi kama ukipambana na timu ikapata ushindi,” alisema Malone.

Che Malone Awataka Wachezaji wenzake Kua Makini Kwenye Mechi ya Watani Jumamosi

Changamoto Zinazokabili Simba

Licha ya mafanikio yao msimu huu, sare dhidi ya Coastal Union imeonyesha udhaifu kwenye safu ya ulinzi ya Simba, kitu ambacho Che Malone ameonya lazima kirekebishwe mara moja. Amebainisha kuwa, licha ya Coastal Union kuwa timu imara, Simba waliruhusu mabao rahisi ambayo hayapaswi kutokea katika mechi kubwa kama hii.

“Tumeruhusu mabao rahisi dhidi ya Coastal Union, tunatakiwa tubadilike. Hatuwezi kurudia makosa yale, tunakwenda kucheza dhidi ya Yanga, na mechi hii ina uzito zaidi,” aliongeza beki huyo wa Simba, akionekana mwenye imani kuwa timu yake itaweza kufanya vyema dhidi ya watani wao.

Simba Kujipanga kwa Ushindi

Simba wakiwa na alama 13 baada ya kushinda michezo minne na kutoka sare moja, wanajua fika kuwa mechi hii ina umuhimu mkubwa katika kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania taji la Ligi Kuu.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, ameeleza kuwa klabu imejipanga vyema kuhakikisha ushindi. “Hii si mechi ya kawaida, ni ya kitamaduni na tunacheza na mpinzani mkubwa.

Ni muhimu kwa wachezaji, mashabiki, na viongozi kushirikiana kuhakikisha tunapata ushindi,” alisema Ahmed.

Akiweka wazi uzito wa mechi hii, Ahmed ameongeza kuwa mechi za dabi zinahitaji umoja wa klabu nzima, kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, hadi mashabiki. Ushindi utahakikisha kuwa Simba inarejesha heshima yake na kuimarisha nafasi yao kwenye mbio za ubingwa wa msimu huu.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Washindi wa Tuzo za Ligi Kuu Ya NBC 2024/2025 Mwezi Septemba
  2. Viingilio Mechi ya Simba VS Yanga 19/10/2024
  3. Fadlu Aanza Mikwara Kuelekea Dabi ya Kariakoo
  4. Max Nzengeli: “Hakuna Dabi Rahisi Duniani Kote”
  5. Ratiba ya NBC Championship Tanzania 2024/2025
  6. Morocco Ahimiza Ubora wa Umaliziaji wa Nafasi Kuelekea Mchezo wa Marudiano na DRC
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo