Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake

Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake

Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake

Mbio za kumsaka bingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake msimu wa 2024/2025 zimeanza kwa kishindo, huku timu za Simba Queens na JKT Queens zikionyesha uwezo mkubwa katika mechi zao za ufunguzi. Jumla ya mabao 12 yamefungwa katika raundi ya kwanza ya ligi kuu ya wanawake Tanzania, na timu hizi zikiwa miongoni mwa zile zilizoweza kupata ushindi mkubwa.

Ushindi wa Simba Queens Dhidi ya Mlandizi Queens

Simba Queens, mabingwa watetezi wa ligi hii, walianza kampeni yao kwa kuonyesha uhodari wa hali ya juu, wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Mlandizi Queens, ambao ni wapya katika michuano hii ya ligi kuu. Mechi hiyo ilifanyika katika Uwanja wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uliopo Kigamboni, Dar es Salaam.

Simba Queen na JKT Queens Waanza na Moto Ligi Kuu wanawake

Kocha mpya wa Simba Queens, Yussif Bagisi kutoka Ghana, alifanikiwa kuongoza timu yake katika ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa msimu, hatua ambayo inatoa taswira nzuri kwa mashabiki na uongozi wa klabu hiyo.

JKT Queens Watoa Kipigo kwa Alliance Girls

Katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, JKT Queens walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Alliance Girls, wakianza msimu kwa kasi. Washambuliaji wa JKT Queens walikuwa moto wa kuotea mbali, huku Winfrida Gerald, Anastazia Katunzi, na mchezaji wa akiba, Janeth Matulanga, wakifunga mabao hayo matatu.

Licha ya Latifa Mustafa kufunga bao la kufutia machozi kwa Alliance Girls, timu hiyo ilishindwa kujiokoa na kipigo hicho cha nyumbani, na JKT Queens wakaondoka na pointi tatu muhimu.

Matokeo Michezo Mingine ya Raundi ya Kwanza

Katika mechi nyingine, Yanga Princess walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Bunda Queens katika Uwanja wa Karume, Mara. Timu ya Bunda Queens, licha ya kucheza pungufu baada ya Jamilah Selestine kuoneshwa kadi nyekundu kipindi cha pili, walipambana na kusawazisha kupitia bao la Melikia William mwishoni mwa mchezo huo.

Wakati huo huo, Ceassia Queens walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate Princess katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Nao Mashujaa Queens na Gets Programme walimaliza mchezo wao kwa suluhu ya 0-0 katika Uwanja wa Major General Isamuhyo, Dar es Salaam.

Raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Wanawake inatarajiwa kuchezwa Jumatatu ijayo, ambapo timu zote kumi zitashuka dimbani kusaka ushindi katika viwanja vitano tofauti nchini. Mchuano huu wa mapema unaleta matumaini makubwa kwa mashabiki wa soka la wanawake, huku timu mbalimbali zikijipanga kuhakikisha zinadumisha ubora kwenye ligi hii yenye ushindani mkali.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Pamba Jiji FC Yafanya Vikao Vizito Baada ya Mwanzo Mbovu Ligi Kuu
  2. Coastal Union Yahamishia Mechi Zake Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha
  3. Msimamo wa Ligi Kuu ya Zanzibar 2024/2025 PBZ premium League
  4. Mario Balotelli Aripotiwa Yupo Karibu Kurudi Italia
  5. Forest Kutoa Ofa ya Mkataba Mpya kwa Wood Kabla ya Uliopo Kumalizika
  6. Dortmund Yamsajili Yan Couto kwa €30 Milioni kutoka Manchester City
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo