Kikosi cha Tanzania Taifa Stars Vs Dr Congo leo 10-10-2024
Timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania, Taifa Stars, leo ipo ugenini kuikabili Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DR Congo) katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Mtanange huu mkali unatarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Stade des Martyrs, Kinshasa, huku kila timu ikiingia uwanjani ikiwa na lengo la kujipatia alama tatu muhimu.
Taifa Stars, chini ya kocha Hemed Suleiman, inajivunia ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wao uliopita, ushindi ambao umewapa morali kubwa kuelekea mchezo wa leo. Hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto kubwa dhidi ya DR Congo, ambao wameanza vyema kampeni za kufuzu kwa kushinda michezo yao miwili ya awali.
Katika mchezo wa leo, Taifa Stars itawakosa baadhi ya wachezaji wake muhimu kutokana na majeraha, lakini kocha Suleiman ametoa kauli ya kujiamini akisema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa mapambano. Amesema kuwa wachezaji wake wamejipanga vyema kimwili na kiakili, na wanafahamu umuhimu wa mchezo huu katika harakati zao za kufuzu fainali za AFCON.
Kwa upande wa DR Congo, kocha Sébastien Desabre ameita kikosi chenye nyota wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya, akiwemo mshambuliaji wa Brentford, Yoane Wissa, na kiungo wa Anderlecht, Edo Kayembe. Huu ni mtihani mkubwa kwa Taifa Stars, lakini pia ni fursa kwao kuonyesha uwezo wao dhidi ya timu bora barani Afrika.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na DR Congo wanasubiri kwa hamu mtanange huu, huku wengi wakitabiri kuwa utakuwa mchezo wa kusisimua na wenye ushindani mkubwa.
Kikosi cha Tanzania Taifa Stars Vs Dr Congo leo 10-10-2024
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania anatarajiwa kutangaza kikosi cha Taifa stars majira ya saa 12. Hapa tutakuletea orodha ya wachezaji wote watakaounda kikosi hicho mara baada ya kutangazwa.
Hiki apa Kikosi cha Taifa Stars leo dhidi ya DR Congo
- Ally Salim (Gk)
- Lusajo Mwaikenda
- Mohamed Hussein
- Ibrahim Abdulla
- Dickson Job
- Adolf Mtasingwa
- Kibu Dennis
- Mudathir Yahya
- Feisal Salum
- Mbwana Samatta [C]
- Clement Mzize
Wachezaji wa Ziada: Yona Jofrey, Zuberi Foba, Abdallah Said, Himid Mao, Pascal Msindo, Bakari Mwamnyeto, Cyprian Thobias, Khalid Habibu, Ibrahim Ame, Nassoro Saadun, Suleiman Mwalimu Coach: Hemed Suleiman
Hiki apa Kikosi chetu cha Utabiri leo
- Ally salum
- Job
- Bacca
- Hussen
- Lusajo
- Mudathir
- Mao
- Kibu
- Fei
- Mzize
- Samatta
Mapendekezo ya Mhariri:
- Msimamo wa Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025
- Cole Palmer Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Mwaka 2023/24
- Ratiba ya Mechi za Kufuzu CHAN 2024 Ukanda wa CECAFA
- Ratiba Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2024/2025
- Chama- Ndoto ya Ubingwa wa Afrika na Yanga Inawezekana!
- Kikao Cha Masaa Saba Man Utd Chamalizika Bila Taarifa ya Hatma ya Ten Hag
- Timu 5 Zinazopewa Nafasi Kubwa Kushindwa Klabu Bingwa Ulaya 2024/2025
Leave a Reply