Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili 2024/2025 ( TCU Second Selection 2024/2025)
Wakati mwaka wa masomo wa 2024/2025 unaendelea kukalibia kuanza, mchakato wa udahili wa wanafunzi kujiunga na vyuo vikuu nchini Tanzania umeingia hatua ya pili, ambapo vyuo vingi tayari vimeanza kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa.
Katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 124,286 walituma maombi yao ya kujiunga na vyuo 86 vilivyoidhinishwa. Mwaka huu, kuna ongezeko la programu za masomo, ambapo 856 zimeidhinishwa ikilinganishwa na 809 mwaka wa masomo uliopita, hivyo kutoa nafasi zaidi kwa waombaji. Jumla ya nafasi za udahili mwaka huu ni 198,986, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.8 kutoka mwaka uliopita. Katika awamu ya kwanza, waombaji 98,890 (asilimia 79.6) walifanikiwa kupata udahili, na idadi hii imeongezeka sana katika Awamu ya Pili.
Wanafunzi waliochaguliwa Katika awamu hii ya pili wanapaswa kuthibitisha udahili wao mara moja ili kuhakikisha nafasi zao zinabaki. Hapa chini habariforum tumekuletea maelezo muhimu kuhusu mchakato huu, takwimu, na hatua zinazopaswa kufuatwa na wanafunzi.
Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili 2024/2025
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itatangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali tarehe 05 Oktoba, 2024. Wanafunzi wanatakiwa kuthibitisha udahili wao kuanzia tarehe hiyo hadi 21 Oktoba, 2024, ili kudumisha nafasi zao.
Ni muhimu kufahamu kwamba kushindwa kuthibitisha udahili ndani ya muda uliowekwa kunaweza kusababisha kupoteza nafasi hiyo na kupewa mwanafunzi mwingine ambae amekosa nafasi katika dirisha la pili la udahili wa vyuo.
Waombaji Waliodahiliwa katika Chuo Zaidi ya Kimoja
Wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga na vyuo zaidi ya kimoja wanatakiwa kuchagua chuo kimoja na kuthibitisha udahili wao. Hii itafanyika kupitia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) au barua pepe. Wale ambao hawataweza kupata ujumbe huo wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa ili kupata namba hiyo ya siri.
Kwa taarifa zaidi, wanafunzi wanaweza kutembelea tovuti rasmi ya TCU ili kupata orodha ya wanafunzi waliochaguliwa katika chuo zaidi ya kimoja Au Soma zaidi kupitia chapisho letu hili Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025 Awamu ya Pili
Awamu ya Tatu ya Udahili wa vyuo Vikuu 2024/2025
Baada ya kukamilika kwa awamu mbili za udahili, TCU imeamua kufungua Awamu ya Tatu ya udahili itakayoanza tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2024. Hii ni fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kupata udahili katika awamu zilizopita. Vyuo vinaelekezwa kutangaza programu ambazo bado zina nafasi ili kuwapa waombaji nafasi ya kujiunga.
Njia za Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga Vyuo vikuu Awamu ya Pili 2024/2025
Wanafunzi wanapaswa kufuatilia kutangazwa kwa majina ya waliochaguliwa kwa karibu. Hapa kuna njia kuu za kuangalia majina haya:
- Kupitia Tovuti ya TCU: Tembelea tovuti rasmi ya TCU www.tcu.go.tz ili kuona orodha ya vyuo vilivyopokea udahili na majina ya wanafunzi waliochaguliwa.
- Tovuti za Vyuo Vikuu: Kila chuo kikuu kitakuwa na orodha ya wanafunzi waliochaguliwa katika tovuti yake. Ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa zote ni sahihi.
- Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS): Wanafunzi wanaweza kupokea ujumbe mfupi kuwajulisha kuhusu udahili wao na hatua zinazofuata.
- Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni: Wanafunzi wanaweza pia kuangalia majina yao kupitia mfumo wa maombi wa mtandaoni kwa kuingia katika akaunti zao walizotumia wakati wa kuomba.
Mapendeklezo ya Mhariri:
Leave a Reply