Orodha ya Majina ya Waliochaguliwa Chuo Cha UDSM Awamu ya Pili 2024/2025 (UDSM Second Selection 2024/2025)
Kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni moja ya hatua kubwa katika safari ya elimu kwa wanafunzi wengi nchini Tanzania. Chuo hiki kinachotambulika kimataifa hutoa fursa za kipekee za kujifunza, kufanya utafiti, na kujijenga kitaaluma. Mwaka wa masomo 2024/2025 umekaribia kuanza, na majina ya waliochaguliwa kujiunga katika awamu ya pili ya udahili yamechapishwa rasmi. Hii ni habari njema kwa wanafunzi ambao hawakupata nafasi katika awamu ya kwanza, kwani sasa wengi wao wamepata nafasi ya kujiunga na chuo hiki.
Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimekamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi katika awamu ya pili kwa mwaka wa masomo wa 2024/2025. Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na programu mbalimbali za masomo zinazotolewa na chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) imetangazwa rasmi, na imeambatanishwa kwa ajili ya umma kuona majina ya waliofanikiwa.
Wanafunzi waliochaguliwa wanapaswa kuthibitisha udahili wao kupitia mfumo rasmi wa udahili wa UDOM (https://application.udom.ac.tz) kuanzia tarehe 5 Oktoba 2024. Barua za udahili zitapatikana pia kupitia akaunti zao za mtandao wa udahili. UDOM inapenda kuwapongeza wote waliochaguliwa na kuwakaribisha kwa moyo mkunjufu kwenye chuo hicho kikubwa na chenye heshima nchini Tanzania.
Namna ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa UDSM Awamu ya Pili (UDSM Second Selection 2024/2025)
Kwa waombaji walioomba kujiunga na UDSM katika dirisha la pili la udahili wa vyuo kwa mwaka 2024/2025, kuna njia kadhaa rahisi za kuangalia kama maombi yao yamekubaliwa na wamechaguliwa katika awamu hii ya pili:
1. Ujumbe Mfupi wa Simu (SMS)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa waombaji waliochaguliwa. SMS hii itakuwa na taarifa muhimu ikiwemo jina la mwanafunzi, kozi aliyochaguliwa, na hatua za kuthibitisha udahili.
Muhimu: Hakikisha namba yako ya simu unayotumia kupokea ujumbe inafanya kazi vizuri na ipo sehemu yenye mtandao mzuri. Ikiwa hujapokea SMS, unaweza kuangalia majina yako kupitia mtandao.
2. Mfumo wa Maombi ya Mtandaoni (Online Admission System)
Waombaji wanaweza pia kuangalia kama wamechaguliwa kupitia mfumo wa mtandaoni wa udahili wa UDSM. Hii ni njia mbadala na rahisi kwa wale ambao hawatapokea SMS au wanahitaji uhakika wa ziada.
- Tembelea tovuti rasmi ya UDSM: https://admission.udsm.ac.tz/.
- Ingia kwenye akaunti yako kwa kutumia jina la mtumiaji na nenosiri.
- Baada ya kuingia, utaona ujumbe unaoonyesha kama umechaguliwa au la.
- Kama umechaguliwa, utaona maelezo ya kozi pamoja na hatua za kuthibitisha udahili.
Uthibitisho wa Udahili kwa Waliochaguliwa Zaidi ya Chuo Kimoja
Wanafunzi waliochaguliwa zaidi ya chuo kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao kwa kuchagua chuo kimojawapo kuanzia tarehe 5 hadi 21 Oktoba 2024. Uthibitisho unapaswa kufanyika kwa kutumia namba maalum ya siri waliyopewa kupitia SMS au barua pepe walizotumia wakati wa kutuma maombi.
Ikiwa mwanafunzi hajapokea namba ya uthibitisho, anashauriwa kuingia kwenye mifumo ya vyuo husika na kuomba ujumbe mfupi wenye namba hiyo maalum. Kwa msaada zaidi, wanaweza kutembelea tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz) ili kuona orodha ya waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja Au Angalia Hapa katika chapisho letu > Majina ya Waliochaguliwa Chuo Zaidi ya Kimoja 2024/2025
Kuthibitisha udahili ni hatua muhimu kwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa.
Mwanafunzi ambaye hatothibitisha udahili wake ndani ya muda uliopangwa, nafasi yake itaondolewa na kutolewa kwa mwanafunzi mwingine. Kwa hivyo, ni muhimu kuhakikisha unathibitisha haraka pindi unapopokea taarifa ya udahili.
Mchakato wa Awamu ya Tatu ya Udahili UDSM
Kwa wale ambao hawakufanikiwa kuchaguliwa katika awamu ya kwanza na ya pili, bado kuna nafasi katika awamu ya tatu. Awamu hii ya mwisho itafunguliwa tarehe 5 hadi 9 Oktoba 2024. Waombaji ambao hawakupata nafasi awamu zilizopita wanahimizwa kutumia fursa hii ya mwisho kuomba udahili kabla ya mwaka wa masomo kuanza rasmi.
Historia Fupi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ni moja ya vyuo vikuu vya zamani zaidi na vyenye heshima kubwa nchini Tanzania. Kilianzishwa mwaka 1961 kama chuo cha tawi la Chuo Kikuu cha London, na baadaye mwaka 1970 kilipata hadhi kamili ya chuo kikuu. UDSM kimeendelea kupanuka na kuwa na vitivo vingi vinavyotoa programu mbalimbali za elimu ya juu.
Leo hii, UDSM kinajivunia kuwa na zaidi ya kozi 100, wahadhiri wenye uzoefu wa hali ya juu, na vifaa bora vya kisasa kwa ajili ya masomo na utafiti. Chuo hiki pia kimechangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya kitaaluma na kijamii nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Soma Pia; Majina ya Waliochaguliwa Chuo Kikuu Cha UDOM Awamu ya Pili 2024/2025
Leave a Reply