Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024 | Kikosi cha Simba leo vs Coastal Union Ligi Kuu ya NBC
Leo, Oktoba 4, 2024, macho na masikio ya mashabiki wa soka nchini Tanzania yataelekezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, ambako wekundu wa msimbazi Simba SC watavaana na wagosi wa kaya Coastal Union kutoka Tanga kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku timu zote zikihitaji ushindi muhimu kwa madhumuni tofauti.
Simba, ikiwa haijafungwa mechi yoyote msimu huu wa Ligi Kuu Bara, inaingia dimbani ikiwa na kikosi thabiti kinachoongozwa na kocha wao Fadlu Davids. Safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi, ikiongozwa na beki mahiri Che Malone Fondoh, haijaruhusu bao lolote kwenye michezo minne iliyopita. Hii inawapa ujasiri mkubwa kuendeleza rekodi hiyo leo dhidi ya Coastal Union.
Wachezaji wengine watakaokuwa wakitegemewa na Simba katika mechi hii ya leo ni pamoja na kiungo mahiri Debora Fernandez, ambaye ameendelea kuwa mchezaji muhimu katika safu ya viungo wa timu hiyo, pamoja na mshambuliaji wao nyota leonel Ateba, anayetarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji kutafuta mabao zaidi.
Kwa upande wa Coastal Union, mshambuliaji wao Maabad Maulid, ambaye tayari ana mabao mawili kwenye ligi msimu huu, ana jukumu kubwa leo la kujaribu kuvunja safu ya ulinzi ya Simba. Maabad, anayetarajiwa kupewa nafasi kubwa ya kuonyesha uwezo wake, amekuwa akifanya mazoezi ya ziada ili kujiandaa kwa mchezo huu mgumu.
Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mechi, Maabad alisema: “Mchezo dhidi ya Simba utakuwa mgumu lakini tuna imani na mbinu tulizojiandaa nazo, nitaingia uwanjani nikiwa na mkakati thabiti wa kukabiliana na mabeki wao.”
Coastal Union inahitaji pointi muhimu ili kuboresha nafasi yao kwenye msimamo wa ligi, hasa baada ya kuanza msimu kwa matokeo yasiyoridhisha, ikishinda mechi moja tu kati ya sita walizocheza.
Kikosi cha Simba vs Coastal Union Leo 04/10/2024
Kikosi cha Simba dhidi ya Coastal Union leo kinatarajiwa kutangazwa rasmi majira ya saa 9 alasiri.
Hapa habariforum tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaotajwa na kocha wa Simba Faldu Davids kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi hii muhimu. Endelea kufuatilia chapisho ili ili kupata taarifa sahihi za kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa.
Takwimu na Rekodi za Mechi Zilizopita
Simba SC inajivunia rekodi nzuri dhidi ya Coastal Union, kwani tangu msimu wa 2019/2020, Simba haijapoteza mchezo wowote dhidi ya Coastal, ikishinda mara 10 kati ya michezo 12 waliyokutana. Msimu huu, Simba imecheza michezo minne, ikishinda yote na kufikisha pointi 12 huku ikifunga mabao 10 bila kuruhusu bao lolote. Hali hii inawafanya kuwa timu inayoshtakiwa zaidi kuelekea mchezo wa leo.
Kwa upande wa Coastal Union, hali yao haijawa nzuri msimu huu, wakiwa na pointi nne tu baada ya kushinda mechi moja, sare moja na kupoteza mechi nne. Hali hii inawasukuma kuhitaji ushindi kwa udi na uvumba ili kujiondoa kwenye nafasi mbaya waliyopo kwenye msimamo wa ligi.
Matarajio na Mbinu za Kocha wa Simba
Kocha Fadlu Davids ameendelea kutilia mkazo utumiaji mzuri wa nafasi wanazozipata wachezaji wake. Katika mahojiano na waandishi wa habari, kocha huyo alisema: “Tumeendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha tunatumia vizuri nafasi zetu za kufunga. Lengo letu ni kuondoka na ushindi mnono leo, hata kama Coastal Union watajaribu kutumia mbinu za kujihami kwa kupaki basi.”
Hii inaashiria kuwa Simba imejipanga vizuri kwa mchezo huu, ikihitaji pointi tatu muhimu ili kuimarisha nafasi yao ya kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply