Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024

Yanga vs Pamba Jiji Leo 03 10 2024 Saa Ngapi

Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Pamba

Leo, tarehe 3 Oktoba 2024, Yanga SC inakutana na Pamba Jiji katika mechi ya Ligi Kuu Bara Tanzania. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, kuanzia saa 12:30 jioni. Hii ni mechi muhimu kwa pande zote mbili, kwani Yanga inataka kuendeleza rekodi yake nzuri huku Pamba Jiji ikitafuta ushindi wake wa kwanza msimu huu.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Miguel Gamondi, ameweka wazi kuwa kikosi chake kinajipanga kushambulia kwa nguvu ili kuvunja ulinzi wa Pamba Jiji. Katika michezo iliyopita ya ligi, Yanga imeweza kufunga mabao manne lakini mashabiki wanatarajia kuona mabao zaidi kutokana na uwezo mkubwa ulioonyeshwa na timu hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Gamondi ameeleza kuwa wapinzani wao, Pamba Jiji, ni timu inayojilinda zaidi kuliko kushambulia, hali inayopelekea Yanga kutumia mbinu za kulazimisha mashambulizi kuhakikisha wanapata ushindi. Akizungumza kabla ya mechi, alisema:

“Tumejipanga kiakili na kimwili kwa mchezo huu. Tunafahamu kwamba Pamba Jiji ni timu imara kwenye ulinzi, lakini tutalazimisha ushindi kwa kushambulia kwa ustadi,” alisema Gamondi.

Yanga imeshinda michezo mitatu ya ligi msimu huu na kufikisha alama 9 bila kuruhusu bao lolote. Ushindi kwenye mchezo wa leo utawafanya kuendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi.

Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024 | Matokeo ya Yanga Leo Dhidi ya Pamba

Matokeo ya Yanga vs Pamba Jiji Leo 03/10/2024

Yanga SCVSPamba Jiji
  • 🏆 #NBCPremierLeague
  • ⚽️ Young Africans SC🆚Pamba Jiji
  • 📆 03.10.2024
  • 🏟 Azam Complex
  • 🕖 6:30PM(EAT)

Pamba Jiji na Mbinu za Kujilinda na Kushambulia

Kwa upande wa Pamba Jiji, licha ya kutokuwa na rekodi nzuri msimu huu, wamejipanga vizuri kwa mechi hii dhidi ya Yanga. Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Henry Mkanwa, ameeleza kuwa wataingia uwanjani wakilenga mbinu za kushambulia na kujilinda kwa ustadi.

Mkanwa amesema kwamba timu yake imekusanya pointi nne kutoka mechi sita, huku wakipoteza mbili na kutoa sare nne. Hata hivyo, bado hawajapata ushindi msimu huu, lakini kocha huyo ana matumaini ya kuvunja mwiko huo leo.

“Mpango wetu uko vizuri, tunaenda kupambana kupata matokeo mazuri, Mungu akipenda tutapata ushindi. Yanga ni timu bora lakini sisi tumejiandaa,” alisema Mkanwa.

Kiungo wa Pamba Jiji, Paulin Kasindi kutoka DR Congo, ameongeza kuwa kikosi chake kipo tayari kupambana bila hofu, na wanaiheshimu Yanga kwa uwezo wao lakini hawatawapa nafasi ya kupata pointi kwa urahisi. “Tunajua Yanga ni timu nzuri, lakini hatutakuja kuwapa pointi tatu kirahisi. Tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,” alisema Kasindi.

Takwimu Muhimu za Timu Kwa Mechi Zilizopita

  • Yanga SC: Imeshinda michezo mitatu ya ligi msimu huu, ikifunga mabao 4 bila kuruhusu bao lolote. Katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, walifanikiwa kuichabanga Vital’O mabao 10-0 na CBE SA mabao 7-0 katika mechi mbili.
  • Pamba Jiji: Katika mechi sita za awali, Pamba Jiji imepata sare nne, kupoteza mbili, huku ikiwa haijashinda hata moja. Imeruhusu mabao matano tu na kufunga mawili.

Matarajio ya Mchezo

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili.

Yanga inatarajiwa kutumia mbinu za kushambulia kwa nguvu, ikilenga kutumia nafasi yoyote ya kufunga mabao. Kwa upande wa Pamba Jiji, watategemea mbinu za kujilinda na mashambulizi ya kushtukiza kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Matarajio ya mashabiki ni kuona Yanga ikiendelea na mwendo wa ushindi, huku Pamba Jiji ikitafuta ushindi wake wa kwanza msimu huu. Mchezo huu utakuwa kipimo kikubwa kwa Yanga SC ambao wanatakiwa kuonyesha uwezo wao wa kushinda michezo muhimu kama hii ili kujiweka vizuri katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vituo vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Pamba jiji 03/10/2024
  2. Viingilio Mechi ya Yanga Vs Pamba jiji 03/10/2024
  3. Ratiba ya Azam FC Ligi Kuu 2024/2024
  4. Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Oktoba 03, 2024
  5. Mashujaa FC Yajinadi Kutinga Nne Bora, Yatoa Angalizo Kwa Singida BS
  6. Viingilio Mechi ya Simba Vs Coastal Union 04/10/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo