Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR

Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR

Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR | Ratiba Mpya Ya Treni ya Umeme Kuanza Kutumika oktoba 01 2024

Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza ratiba mpya ya safari za Treni ya Mwendokasi ya SGR (Standard Gauge Railway) ambayo itaanza kutumika kuanzia tarehe 1 Oktoba 2024. Treni hizi zitaunganisha jiji la Dar es Salaam, Morogoro, na Dodoma kwa haraka zaidi na ufanisi wa hali ya juu, huku zikilenga kuboresha huduma za usafiri nchini.

Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR: Dar – Morogoro – Dodoma

Kwa mujibu wa ratiba mpya, kuna treni za aina mbili zinazotolewa: Haraka (Express) na Kawaida (Ordinary). Ratiba hizi zinajumuisha muda wa kuondoka na kufika kwa treni kati ya vituo vikuu vya Dar es Salaam (DSM), Morogoro (MOR), na Dodoma (DOM).

1. Treni ya Haraka (Express)

Treni za haraka zinajulikana kwa kasi yake na muda mfupi wa safari. Ratiba ya safari za Treni ya Haraka ni kama ifuatavyo:

  • Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
    • Saa 12:00 Asubuhi
    • Saa 11:15 Alfajiri
  • Kuwasili Morogoro (MOR):
    • Saa 1:40 Asubuhi kwa treni ya saa 12:00 Asbh
    • Saa 1:12 Asubuhi kwa treni ya saa 11:15 Alfajiri
  • Kuondoka Morogoro:
    • Saa 1:45 Asubuhi
    • Saa 1:17 Asubuhi
  • Kuwasili Dodoma (DOM):
    • Saa 3:42 Asubuhi kwa safari ya treni ya saa 12:00 Asbh
    • Saa 2:53 Asubuhi kwa safari ya saa 11:15 Alfajiri

2. Treni ya Kawaida (Ordinary)

Treni za kawaida huchukua muda mrefu zaidi kutokana na kuacha katika vituo vingi njiani. Ratiba ya safari hizi ni kama ifuatavyo:

  • Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
    • Saa 3:30 Asubuhi
  • Kuwasili Morogoro (MOR):
    • Saa 5:15 Asubuhi
  • Kuondoka Morogoro:
    • Saa 5:20 Asubuhi
  • Kuwasili Dodoma (DOM):
    • Saa 7:25 Mchana

Pia, kuna safari za kawaida kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam:

  • Kuondoka DOM (Dodoma):
    • Saa 8:10 Mchana
    • Saa 11:15 Jioni
    • Saa 12:55 Usiku

Safari hizi husababisha kufika Morogoro kati ya saa 10:15 Jioni hadi saa 2:51 Usiku, na kutoka hapo kuelekea DSM kwa nyakati tofauti kulingana na safari iliyochaguliwa.

Ratiba Mpya ya Treni ya Kawaida Dar es Salaam – Morogoro

Kwa wale wanaosafiri kati ya Dar es Salaam na Morogoro pekee, kuna huduma za treni za kawaida zenye ratiba ifuatayo:

  • Kuondoka Morogoro (MOR):
    • Saa 3:50 Asubuhi
  • Kuwasili Dar es Salaam (DSM):
    • Saa 5:40 Asubuhi
  • Kuondoka DSM (Dar es Salaam):
    • Saa 10:00 Jioni
  • Kuwasili Morogoro (MOR):
    • Saa 11:40 Jioni

Ratiba Mpya ya Treni Za Mwendokasi SGR

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Nauli za Mabasi ya Mikoani 2024 LATRA
  2. Hizi apa Bei Mpya Vifurushi vya Azam 2024
  3. Nauli za Treni ya Mwendokasi SGR 2024
  4. Nauli ya Treni ya Umeme ya SGR Dar to Dodoma
  5. Ratiba ya Treni ya Mwendokasi Ya SGR 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo