Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid

Mshambuliaji nyota wa PSG, Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid

Nyota wa soka wa Ufaransa, Kylian Mbappe, amethibitisha kuwa ataondoka Paris Saint-Germain (PSG) mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na klabu ya ndoto yake, Real Madrid. Uhamisho huu umekuwa gumzo kubwa katika ulimwengu wa soka, hasa kwa sababu Mbappe yuko tayari kupunguza mshahara wake kwa kiasi kikubwa ili kutimiza ndoto yake.

Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid

Mbappe Akubali Punguzo Kubwa la Mshahara Ili Kujiunga na Real Madrid

Mbappe, mwenye miaka 24, ambaye mkataba wake na PSG unakamilika mwishoni mwa msimu huu, ametangaza wiki iliyopita kwamba ataondoka PSG. Mfaransa huyo anatarajiwa kusaini mkataba na Real Madrid.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, Mbappe amekuwa akipokea mshahara wa jumla ya €72 milioni (£62 milioni) kwa mwaka akiwa PSG. Hata hivyo, ili kujiunga na Real Madrid, Mbappe atakubali mshahara wa €25 milioni (£21 milioni) kwa mwaka baada ya kodi. Hili ni punguzo la zaidi ya asilimia 60 kutoka mshahara wake ambao alikua nalipwa akiichezea miamba ya soka ya Ufaransa PSG.

Mbali na hilo, atapokea bonasi ya kusaini ya pauni milioni 129.2, ambayo inasemekana kulipwa kwa miaka mitano.

Mbappe atakuwa mchezaji mwenye mshahara mkubwa zaidi katika kikosi cha Real Madrid, na pia anatarajiwa kupokea bonasi kubwa ya kusaini, huku Los Blancos wakilazimika kutolipa ada ya uhamisho.

Sababu Za Mbappe Kukubali Punguzo Hili

Sababu kuu ya Mbappe kukubali punguzo hili kubwa la mshahara ni ndoto yake ya kucheza katika klabu bora Duniani Real Madrid. Tangu akiwa mtoto, Mbappe amekuwa shabiki mkubwa wa Ronaldo na Real Madrid na ameonyesha wazi nia yake ya kuchezea klabu hiyo.

Zaidi ya hayo, Real Madrid inatoa fursa kubwa kwa Mbappe kushinda mataji makubwa, ikiwa ni pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA Champions legue. Hii ni jambo ambalo Mbappe anaamini kuwa halikuwa rahisi kufikia akiwa PSG ambao wamekua wakiishia katika hatua ya nusu fainali na robo fainali kwa misimu yote tangu ajiunge PSG.

Mabadiliko Katika Mfumo wa Real Madrid

Kuwasili kwa Mbappe kunaweza kusababisha mabadiliko katika mfumo wa uchezaji wa Real Madrid. Kocha Carlo Ancelotti huenda akaamua kutumia mfumo wa 4-3-3 ili kumpa nafasi Mbappe kucheza katika nafasi yake anayoipenda ya winga wa kushoto.

Mwisho

Uhamisho wa Kylian Mbappe kwenda Real Madrid unaonyesha kuwa fedha sio kila kitu katika soka. Ndoto na hamu ya kushinda mataji vinaweza kuwa vichocheo vikubwa zaidi. Mashabiki wa soka kote duniani wanasubiri kwa hamu kuona jinsi Mbappe atakavyong’ara akiwa katika jezi nyeupe ya Real Madrid.

Habari Nyengine: Kylian Mbappé Atangaza Kuondoka PSG Huku Kukiwa na Tetesi za Kujiunga Real Madrid

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo