Manchester United Yapigwa Tena Nyumbani, Hali Yazidi Kuwa Ngumu Old Trafford

Manchester United Yapigwa Tena Nyumbani, Hali Yazidi Kuwa Ngumu

MANCHESTER, ENGLAND: Hali imeendelea kuwa ngumu kwa Manchester United, baada ya jana kuchapwa mabao 3-0 na Tottenham kwenye Uwanja wa Old Trafford na kuendelea kushuka kwenye msimamo.

Huu ni mchezo wa sita kwa Man United ikishinda miwili, sare moja na kupoteza mitatu na jioni ya jana ilishuhudia ikicheza pungufu baada ya nahodha wake Bruno Fernandez kupewa kadi nyekundu.

Mabao ya Spurs yaliwekwa kimiani na Brennan Johnson dakika ya tatu ya mchezo, kabla ya Dejan Kulusevski kuweka la pili dakika ya 47 na Dominic Solanke kupigilia msumari wa mwisho dakika ya 77.

Huu ni mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya Uingereza kupoteza nyumbani msimu huu baada ya wa kwanza Old Trafford kuchapwa mabao 3-0 na Liverpool na imeshuka hadi nafasi ya 12 ikiwa na pointi saba. Spurs imepanda hadi nafasi ya nane baada ya michezo sita na ina pointi 10 ikishinda mitatu sare moja na kupoteza miwili.

Manchester United Yapigwa Tena Nyumbani, Hali Yazidi Kuwa Ngumu Old Trafford

Kocha wa Man United ana kazi ya kufanya kulinda kibarua chake licha ya mabosi wa miamba hiyo kuonekana wanamwamini kwa sasa. Hata hivyo matokeo mabaya inayoendelea kupata inaweza ikabadilisha mambo kwenye viunga vya Carrington na akafunguliwa milango ya kutokea.

Mchezo mwingine uliopigwa jana ni wa Ipswich dhidi ya Aston Villa ikishuhudiwa sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Portman Road.

Liam Delap aliifungia mabao mawili Ipswich huku ya Villa yakifungwa na Ollie Watkins na Morgan Rogers.

Matokeo hayo yameifanya wenyeji Ipswich kuwa nafasi ya 15 baada ya michezo sita ikiwa haijashinda hata mmoja ina sare nne na kupoteza miwili. Villa imecheza pia michezo sita na imeshinda minne, sare moja na kupoteza mmoja ikiwa na pointi 13.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Ahoua Aipa Simba Pointi Tatu Muhimu Uwanja wa Jamhuri
  2. Matokeo ya Yanga Vs KMC Leo 29 September 2024
  3. Matokeo ya Simba Sc vs Dodoma Jiji Leo 29/09/2024
  4. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  5. Simba SC kuwakosa Mutale, Kagoma na Mzamiru Dhidi ya Dodoma Jiji
  6. Ratiba ya Mechi za Ligi Kuu ya NBC Leo Septemba 29, 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo