FIFA Yaitandika Yanga Faini Nzito Kufuatia Kesi ya Okrah

FIFA Yaitandika Yanga Faini Nzito Kufuatia Kesi ya Okrah

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeipa Yanga SC adhabu nzito baada ya kuamuru klabu hiyo ya Dar es Salaam kumlipa mchezaji Augustine Okrah fidia ya dola 24,000 (sawa na shilingi za Kitanzania milioni 65.6) pamoja na faini ya dola 3,000 (takriban shilingi milioni 8.2). Hatua hii inatokana na mgogoro wa kimkataba kati ya klabu hiyo na winga huyo kutoka Ghana.

Mzozo huu ulianza baada ya Augustine Okrah, aliyesajiliwa na Yanga kwa msimu wa 2022/2023, kudai kuwa klabu hiyo ilikiuka baadhi ya masharti ya mkataba wake, ikiwemo suala la malipo.

Baada ya Okrah kufikisha malalamiko yake FIFA, kamati ya usuluhishi ya shirikisho hilo ilifanya uchunguzi wa kina na kubaini kuwa Yanga haikuheshimu vipengele muhimu vya mkataba huo, jambo lililopelekea maamuzi haya dhidi ya mabingwa hao wa Tanzania.

FIFA, katika maamuzi yake, ilibainisha kuwa Yanga SC wanapaswa kumlipa Okrah fidia hiyo ndani ya siku 30. Hii ni baada ya kukubaliana kuwa mchezaji huyo ana haki ya malipo hayo kutokana na ukiukwaji wa makubaliano yaliyowekwa awali na pande zote mbili.

Yanga SC inakabiliwa na adhabu kubwa zaidi iwapo watashindwa kufuata agizo hili la FIFA ndani ya muda uliowekwa. Ikiwa klabu hiyo itashindwa kumlipa Okrah ndani ya siku 45, wanaweza kupewa vikwazo vikali zaidi ambavyo vitakuwa pigo kubwa kwao. Moja ya adhabu kubwa zaidi ni kufungiwa kusajili wachezaji wapya kwa madirisha matatu ya usajili.

FIFA Yaitandika Yanga Faini Nzito Kufuatia Kesi ya Okrah

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mbeya City Yaibuka na Ushindi wa 1-0 Dhidi ya Mbeya Kwanza
  2. Moussa Camara Ajivunia Kamati ya Ulinzi Simba
  3. Simba Yaamishia Majeshi ya Usajili Kwa Fei Toto Baada ya Mpanzu
  4. Vituo Vya Kununua Tiketi za Mechi ya Yanga Vs KMC 29.09.2024
  5. Hivi Apa Viingilio Mechi ya Yanga vs KMC 29.09.2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo