Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024

Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024 | Kikosi cha Azam Leo Vs Simba Ligi Kuu ya NBC 

Leo, tarehe 26 Septemba 2024, mashabiki wa mpira wa miguu watashuhudia mtanange mkubwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wana rambaramba Azam FC na wekundu wa msimbazi Simba SC katika uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Hii ni miongoni mwa mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa, kwani timu hizi mbili zimekuwa na ushindani wa muda mrefu tangu Azam ilipopanda daraja mwaka 2008.  Azam na Simba zimekutana mara 32 tangu Azam ilipoanza kushiriki Ligi Kuu.

Katika mechi hizo, Simba imeibuka kuwa mbabe kwa kushinda mara 14 huku Azam ikishinda mara 6 pekee. Mechi 12 kati ya hizo zimeisha kwa sare, na Simba inaongoza kwa kufunga mabao mengi zaidi—44 dhidi ya 29 ya Azam.

Simba imeweza kudhihirisha ubabe wake zaidi dhidi ya Azam katika mechi za ugenini. Kwa upande wa Azam, nyumbani imekuwa ikipoteza mara nyingi zaidi, hali inayoonesha changamoto kubwa inazokutana nazo zinapokutana na wapinzani wao wakubwa, Simba.

Mechi ya leo itawakutanisha makocha wapya wa timu zote mbili; Rachid Taoussi wa Azam na Fadlu Davids wa Simba. Huu ni msimu wa kwanza kwa makocha hawa kuiongoza timu zao kwenye ligi, na tayari wameanza kuonyesha mwelekeo mzuri.

Azam FC chini ya kocha Taoussi, imeanza msimu vizuri kwa kupata alama saba katika mechi tatu za kwanza. Miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuleta ushindani ni kiungo mkabaji, James Akaminko, na washambuliaji Adolf Mtasingwa na Ever Meza, ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha timu yao inakuwa na matokeo mazuri.

Kwa upande wa Simba SC, kocha Davids amewaongoza vizuri wachezaji wake na timu hiyo tayari imepata ushindi katika mechi zake mbili za mwanzo. Miongoni mwa wachezaji muhimu wa Simba ni Jean Charles Ahua, kiungo fundi ambaye ameonesha uwezo mkubwa, pamoja na mshambuliaji Debora Mavambo aliyekuwa katika kiwango bora kwenye mechi za CAF zilizopita. Pia wachezaji kama Valentino Mashaka na Lionel Ateba wamesaidia kuimarisha kikosi na wanatarajiwa kuleta changamoto kwa Azam leo usiku.

Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024

Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024

Kikosi cha Azam kitakacho ikabiri Simba sc katika mchezo huu kinatarajiwa kutangazwa rasmi leo majira ya saa moja usiku.

Hapa tutakuletea orodha kamili ya wachezaji wote watakaotajwa na kocha wa Azam Sc kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kwa ajili ya mechi hii muhimu. Endelea kufuatilia chapisho ili ili kupata taarifa sahihi za kikosi hicho mara tu kitakapotangazwa.

Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024
Kikosi cha Azam Vs Simba Leo 26/09/2024

Rekodi za Mechi za Awali Kati ya Azam vs Simba

Katika msimu uliopita, timu hizi zilikutana mara mbili na Simba ilifanikiwa kupata ushindi mkubwa wa mabao 3-0 katika mechi ya mwisho ya msimu. Azam itatafuta kulipiza kisasi kwenye mchezo wa leo huku Simba ikitazamia kuendeleza utawala wake. Aidha, mechi ya leo itakuwa ya tatu kuchezwa nje ya Dar es Salaam, baada ya mechi mbili zilizotangulia kuchezwa Tanga na Mwanza.

Je, Leo Mambo Yatakuwa Vipi?

Wakati wa mchezo huu, mashabiki watakuwa na matumaini makubwa kwa timu zao kuona nani atatoka kifua mbele. Ushindani kati ya timu hizi mbili umejikita zaidi kwenye ubora wa viungo, na hii ni kutokana na uwezo wa wachezaji wa katikati ya uwanja. Kikosi cha Azam kinaweza kutegemea uimara wa wachezaji wake wa kiungo kama Feisal Salum (Fei Toto) na James Akaminko, wakati Simba inategemea ubunifu wa Jean Charles Ahua na kasi ya winga Lionel Ateba.

Hii ni moja ya mechi inayotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na historia ya timu hizi na ubora wa vikosi vyao kwa msimu huu. Kwa mashabiki, usiku huu utakuwa wa kusisimua, huku Azam ikijitahidi kupata ushindi mbele ya Simba ambayo imeonekana kuwa na rekodi nzuri dhidi ya wapinzani wao.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo Kengold Vs Yanga Sc Leo 25/09/2024
  2. Fadlu David na Simba SC Wamejipanga Vyema Kukabiliana na Azam FC Kesho
  3. JKT Tanzania VS Coastal Union Leo 25/09/2024 Saa Ngapi?
  4. Kengold Wakijichanganya Tunawapiga Nyingi, Gamondi Atoa Onyo
  5. Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba
  6. Takwimu za Chama Yanga zaanza kutisha Klabu Bingwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo