Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba

Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba

Wakati ukuta unazidi kuyeyuka kuelekea pambano la kukata na shoka kati ya Azam FC na Simba SC, macho na masikio ya mashabiki wa soka Tanzania yameelekezwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Mchezo huu, ukiwa ni sehemu ya mchuano wa Ligi Kuu Bara, umeweka matumaini na hofu kwa pande zote mbili, huku rekodi za zamani zikionesha Simba kuwa na ubabe dhidi ya Azam.

Azam FC Kwenye Mtihani Mzito Zanzibar Dhidi ya Simba

Historia na Takwimu Zinavyo kandamiza Azam

Kihistoria, Azam FC imekuwa na wakati mgumu inapokutana na Simba SC, hususan katika michezo ya Ligi Kuu Bara.

Tangu Azam ilipoanza kushiriki ligi hiyo mwaka 2008, timu hizi zimekutana mara 32 ambapo Azam imeshinda mara 6 pekee, ikipata sare 12 na Simba kushinda mara 14. Katika mechi za hivi karibuni, Simba imeendeleza ubabe wake, ambapo kwenye fainali ya Kombe la Muungano mwaka huu, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na nyota wao wa zamani, Babacar Sarr.

Zaidi ya hayo, mchezo wa mwisho wa ligi baina ya timu hizi ulifanyika Mei 9, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo Simba iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0, yaliyotiwa nyavuni na Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma, na David Kameta ‘Duchu’. Ushindi huo uliimarisha zaidi udhibiti wa Simba katika mechi zao dhidi ya Azam.

Mkakati wa Azam Kuelekea Mtihani Mzito Zanzibar

Licha ya rekodi hizo za nyuma kumweka Azam FC katika nafasi ukibonde mbele ya Simba, hali ya sasa inatoa hamasa kwa kikosi hicho kinachoongozwa na kocha mpya, Rachid Taoussi. Taoussi, ambaye alichukua mikoba ya Youssouph Dabo aliyeondolewa kutokana na mwenendo mbaya, ameonesha dalili nzuri ya kubadili upepo na kurejesha morali ya ushindi kwa kikosi cha Azam ambapo katika mechi za hivi karibuni, Azam imefanikiwa kushinda michezo miwili mfululizo dhidi ya KMC na Coastal Union.

Moja ya silaha kubwa ya Azam FC katika mchezo huu ni uwezo wake wa kushambulia kwa haraka na kuzuia kwa nidhamu. Katika mchezo uliopita dhidi ya Coastal Union, Azam iliweza kuonesha nidhamu ya hali ya juu kwenye safu ya ulinzi na kufunga bao la ushindi katika dakika za mwisho. Hii inatoa matumaini kuwa huenda wakaweza kuvunja mwiko wa kushindwa mara kwa mara na Simba.

Simba SC na Lengo la Kuendeleza Ubabe

Kwa upande wa Simba SC, klabu hiyo iko katika ubora unaorizisha chini ya kocha wao mpya, Fadlu Davids, ambaye ameshinda michezo yote miwili ya Ligi Kuu Bara aliyoiendesha. Simba imeonekana kuwa na safu ya ushambuliaji ya hatari, huku ikipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tabora United na mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate.

Simba pia imeimarika zaidi kwa kusajili wachezaji wa kiwango cha juu, kama vile Fabrice Ngoma na Sadio Kanoute, ambao wamekuwa muhimu katika kuendesha safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Aidha, Simba ina uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kucheza kwa kasi, jambo linalowapa nafasi kubwa ya kushinda kwenye mchezo huu dhidi ya Azam.

Kutakua na Nini Zanzibar?

Kile kinachosubiriwa kwa hamu kubwa ni kuona kama Azam FC itapata nguvu ya kuvunja mwiko wa kushindwa mara kwa mara dhidi ya Simba, au kama Simba itaendeleza ubabe wake katika mechi hii ya kiporo. Mchezo huu utakuwa wa kipekee kwa sababu unachezwa katika uwanja wa New Amaan, Zanzibar, ambao unatoa changamoto tofauti ikilinganishwa na viwanja vya Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, matokeo ya mchezo huu yatakuwa na athari kubwa kwenye msimamo wa ligi, huku timu zote mbili zikiwa na malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara. Ushindi kwa Azam utawapa nguvu na kujiamini zaidi, wakati Simba wakihitaji ushindi kuendelea kujiweka kileleni na kuimarisha nafasi yao ya kutwaa taji.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Takwimu za Chama Yanga zaanza kutisha Klabu Bingwa
  2. Hizi Ndio Timu 5 Ambazo Bado Hazijashinda Mechi yoyote Ligi Kuu
  3. Aziz KI Afichua Kilichomo Kwenye Mkataba Wake na Yanga
  4. Ratiba ya Mechi ya Leo 25 September 2024
  5. Kengold Vs Yanga Leo 25/09/2024 Saa Ngapi
  6. Timu Zilizofuzu Makundi CAF 2024/2025
  7. Timu zilizofuzu Makundi Kombe La Shirikisho CAF 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo