Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024 | Tangazo La Kuripoti Shule Ya Polisi Moshi Kwa Vijana Waliochaguliwa Kujiunga Na Jeshi La Polisi Tanzania | Waliopata Kazi za Polisi September 2024

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Jeshi la Polisi Tanzania limekuwa likipokea maombi kutoka kwa vijana wa Kitanzania wenye sifa za kujiunga na kikosi hicho ili kupata mafunzo maalum yanayowandaa kwa ajili ya kutumikia taifa.

Kila mwaka, Jeshi la Polisi hufanya usaili wa kuchagua vijana wenye vigezo vinavyostahili, na kwa mwaka 2024, mchakato huu umekamilika, na majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi yametangazwa rasmi.

Kwa mwaka 2024, Jeshi la Polisi Tanzania limechagua kundi jipya la vijana ambao watakuwa sehemu ya mafunzo ya awali ili kuwa askari wa Jeshi la Polisi. Katika makala hii, tumekuletea orodha kamili ya waliochaguliwa kujiunga na jeshi la Polisi, taarifa kamili kuhusu utaratibu wa kuripoti kwa vijana walioteuliwa, masharti ya kujiunga na mafunzo, na vifaa wanavyopaswa kuwa navyo. Kwa wale wote waliopata nafasi hii ya kipekee, ni muhimu kufahamu maelekezo haya ili kuhakikisha mchakato wa kuripoti unaenda kwa mpangilio sahihi.

Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Taarifa Muhimu kwa Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Kwa mujibu wa tangazo rasmi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, vijana wote waliofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya Polisi wanapaswa kuzingatia tarehe na mahitaji maalum kabla ya kuripoti kwenye Shule ya Polisi Moshi kwa ajili ya kuanza mafunzo yao. Hii ni nafasi ya kipekee kwa vijana kujiandaa kutumikia taifa na kupata mafunzo muhimu ya kiulinzi na usalama.

Tarehe za Kuripoti Shule ya Polisi Moshi

Vijana waliochaguliwa wanatakiwa kufika Shule ya Polisi Moshi kati ya tarehe 30 Septemba 2024 hadi 02 Oktoba 2024. Ni muhimu kwa waliochaguliwa kuhakikisha wanaripoti kwa wakati ili kuepuka kuhesabiwa kama wamejiondoa wenyewe kwenye mafunzo. Mtu yeyote atakayeripoti baada ya tarehe 02 Oktoba 2024 hatapokelewa.

  • Waliochaguliwa kutoka Dar es Salaam: Wanaotakiwa kuripoti DPA na vikosi vya Makao Makuu ya Polisi wanapaswa kufika katika eneo la Polisi (Barracks) Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam, tarehe 30 Septemba 2024 saa 12 asubuhi ili kuanza safari ya kuelekea Moshi.
  • Waliochaguliwa kutoka mikoa ya Tanzania Bara: Wanapaswa kuripoti kwa makamanda wa mikoa husika tarehe 29 Septemba 2024, saa 2 asubuhi ili kupatiwa utaratibu wa kusafiri.
  • Waliochaguliwa kutoka Zanzibar: Vijana waliofanyiwa usaili Zanzibar wanapaswa kuripoti Makao Makuu ya Polisi Zanzibar (Ziwani) tarehe 29 Septemba 2024 kwa utaratibu wa safari kwenda Moshi.

Masharti na Vifaa Muhimu kwa Mafunzo

Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na mafunzo wanatakiwa kuwa na vifaa muhimu kwa ajili ya maisha ya chuoni. Hii ni pamoja na:

  1. Vifaa vya kuvaa:
    • Track suit ya rangi ya bluu yenye ufito mweupe,
    • Fulana nyeupe isiyo na maandishi,
    • Raba nyeusi,
    • Soksi nyeusi, na
    • Bukta mbili za michezo za rangi ya bluu.
  2. Vifaa vya malazi:
    • Chandarua cheupe cha duara,
    • Shuka mbili za rangi ya light blue (jumla shuka nne),
    • Blanketi la kijivu lisilo na maua, na
    • Pasi ya mkaa.
  3. Vifaa vya usafi na kazi:
    • Reki,
    • Jembe lenye mpini,
    • Panga,
    • Ndoo mbili ndogo, na
    • Fagio la chelewa.
  4. Vifaa vya usalama na utambulisho:
    • Kadi ya bima ya Afya (NHIF) au Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi,
    • Vyeti halisi vya taaluma,
    • Cheti halisi cha kuzaliwa,
    • Kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa,
    • Nakala za NIDA za wazazi na watu wa karibu,
    • Picha za passport size sita (background blue), na
    • Nakala tano za kila cheti kilichoainishwa.
  5. Fedha ya kujikimu pia inahitajika kwa matumizi ya kibinafsi wakati wa mafunzo.

Marufuku ya Simu za Mkononi

Ni muhimu kutambua kwamba simu za mkononi haziruhusiwi kabisa chuoni. Yeyote atakayekutwa na simu katika Shule ya Polisi Moshi atachukuliwa hatua za kinidhamu ambazo zinaweza kusababisha kufukuzwa mafunzo mara moja. Shule itatoa utaratibu wa mawasiliano kwa walioko chuoni.

Onyo kwa Wasioripoti kwa Wakati

Kwa vijana wote waliochaguliwa, ripoti Shule ya Polisi Moshi kabla ya tarehe 02 Oktoba 2024 ni agizo la msingi.

Mtu yeyote atakayeshindwa kufika kwa wakati hatapokelewa na itachukuliwa kuwa amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo. Hivyo, ni muhimu kuzingatia tarehe na mahitaji yote yaliyotangazwa ili kuepuka athari za kutopokea mafunzo.

Kanuni za Nidhamu na Uraia

Mafunzo katika Shule ya Polisi Moshi yana nidhamu kali. Ni marufuku kabisa kwa wanafunzi kuripoti na simu za mkononi. Simu itakayoonekana itachukuliwa kama utovu wa nidhamu, na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzoni mara moja. Aidha, mafunzo haya yanasisitiza nidhamu ya hali ya juu, uwajibikaji, na uadilifu ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa askari bora wa baadaye.

Historia Fupi ya Jeshi la Polisi Tanzania

Jeshi la Polisi Tanzania lilianzishwa rasmi mnamo tarehe 25 Agosti 1919, kupitia tangazo la Serikali ya Kiingereza lililotolewa katika gazeti la serikali kwa jina la Jeshi la Polisi Tanganyika. Tangu kuanzishwa kwake, Jeshi la Polisi limeendelea kuwa na jukumu muhimu katika kulinda usalama wa raia na mali zao, huku likikua na kuimarika zaidi kwa miaka.

Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Ili Kuangalia orodha ya waliochaguliwa jeshi la Polisi Tanzania, Bofya Kiungo kilichopo hapa chini.

Pakua hapa Tangazo la Majina ya Waliochaguliwa Kujiunga na Jeshi la Polisi 2024

Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo