Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

7Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024 | Matokeo ya Yanga Leo Vs CBE Kombe la Shirikisho

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania, Yanga SC, leo watawakalibisha CBE SA katika mchezo wa marudiano wa raundi ya pili kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAF. Mechi hii itaanza majira ya saa 02:30 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, na inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka kote nchini Tanzania.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Addis Ababa, Yanga ilishinda 1-0, lakini ushindi huo haukutosheleza kwa mashabiki wengi, kwani timu hiyo ilitengeneza nafasi nyingi lakini ikatumia moja tu. Kwa matokeo hayo, Yanga inahitaji sare tu leo ili kufuzu, lakini wachezaji na benchi la ufundi wanataka zaidi – ushindi wa mabao mengi ili kutuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao wa Afrika.

Baada ya kurejea kutoka Ethiopia, Yanga SC imefanya mazoezi ya kina, hasa katika kuongeza ufanisi wa safu ya ushambuliaji.

Timu imeweka kipaumbele kwenye mazoezi ya kufunga mabao, si kwa washambuliaji pekee bali pia kwa viungo na mabeki, kuhakikisha kuwa kila nafasi inatumika ipasavyo. Lengo kuu ni kuwa na rekodi bora na kuipa heshima klabu yao, huku mashabiki wakiwa na matarajio makubwa kwa wachezaji wao.

Nahodha msaidizi wa timu hiyo, Dickson Job, amesisitiza kuwa kikosi kiko tayari na kila mmoja amejiandaa kuonyesha uwezo bora uwanjani. “Tumejifunza kutokana na mechi ya kwanza. Kila mmoja wetu anataka kuhakikisha tunashinda kwa kishindo, tumejipanga vyema, na leo mashabiki wetu watapata kile wanachokitaka,” alisema Job.

Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Matokeo ya Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024

Yanga Sc 6-0 CBE SA
  • Mchezo Umeanza
  • Dakika 05 Yanga o-0 CBE
  • Chama Amaifungia Yanga Goli la kwanza dakika ya 35
  • Dakika 38 Yanga 1-0 CBE ⚽️
  • Mapumziko, Yanga 1-0 CBE
  • Kipindi Cha Pili Kimeanza
  • Dakika 46, Mzize Anatia Chima ya Pili ⚽️
  • DAkika ya 56, yanga wanafanya Mabadiliko | Anatoka Pacome Anaingia Azizi | Ametoka Max Ameingia Abuya
  • Dakika ya 65 Anatoka Mzize ameingia Dube
  • Dakika ya 74 Aziz Ki anatia chuma ya tatu ⚽️
  • Dakika ya 87 Mudathir Anatia chuma ya nne ⚽️
  • Dakika ya 91 Abaya anaifungia Yanga Goli la 5 ⚽️
  • Aziz Ki Anatia Chuma ya 6, Dakika ya 93 ⚽️
  • Mchezo Umeisha; Yanga 6-0 CBE
  • 🏆 #CAFCL
  • ⚽️ Young Africans SC🆚CBE FC
  • 📆 21.09.2024
  • 🏟 Amaan Complex
  • 🕖 8:30PM(EAT)

Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya CBE SA

Hiki Apa Kikosi cha Yanga Leo Dhidi ya CBE SA

Rekodi za Yanga Katika Mashindano ya CAF

Ikiwa Yanga itaifunga CBE leo, itakuwa mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara mbili mfululizo, jambo ambalo linaongeza hamasa kwa wachezaji na mashabiki. Msimu uliopita, Yanga ilifika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo, na ndoto za msimu huu ni kuvuka mbali zaidi.

Katika historia yao dhidi ya timu za Ethiopia, Yanga imeonyesha rekodi bora, ikiwa imeshinda mara nyingi kuliko kupoteza. Mwaka 1969, Yanga ilishinda kwa mabao 5-0 dhidi ya Saint-George, na mara kadhaa baadaye timu hiyo imeendelea kuwa tishio kwa timu za Ethiopia. Rekodi hii inaongeza shinikizo kwa CBE, timu ambayo inafahamu kuwa Yanga ni wapinzani wa kufuatilia kwa makini.

CBE: Kipeperusha Bendera ya Ethiopia

CBE imefika Zanzibar mapema, ikiwa na matumaini ya kupindua matokeo licha ya kupoteza mchezo wa kwanza nyumbani. Kocha wa timu hiyo, Sisay Kumbe, ameeleza kuwa wamejifunza mengi kutoka mechi ya kwanza na wanaamini bado wana nafasi ya kusonga mbele. “Soka lina chochote kinaweza kutokea, tumefanya maandalizi na tuko tayari kwa changamoto,” alisema Kumbe.

Kwa CBE, mechi hii ni nafasi ya kujitengenezea jina kubwa, na wanahitaji ushindi ili kufuzu. Licha ya changamoto ya kucheza mbele ya mashabiki wengi wa Yanga, kocha huyo amesisitiza kuwa kikosi chake kiko tayari kupambana hadi dakika ya mwisho.

Maandalizi ya Mwisho Kabla ya Mechi ya Yanga vs CBE

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha kuwa wanapata ushindi mzuri nyumbani. “Timu ya CBE sio rahisi kama watu wanavyodhani, lakini tumejiandaa kuhakikisha kuwa tunatumia nafasi nyingi tulizotengeneza,” alisema Gamondi.

Mchezo huu utaongozwa na mwamuzi Abdel Aziz Bouh kutoka Mauritania, ambaye anajulikana kwa kuendesha mechi kadhaa za Yanga hapo awali. Bouh aliwahi kusimamia mchezo wa Yanga dhidi ya TP Mazembe, ambao mabingwa hao wa Tanzania walishinda kwa mabao 3-1.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Kikosi cha Yanga Vs CBE SA Leo 21 September 2024
  2. Ley Matampi Ajitoa Mapema Mbio za Kipa Bora
  3. Picha za Jezi Mpya za Pamba Fc 2024/2025
  4. Taoussi Atuliza Presha Kabla ya Azam Kukipiga na Coastal
  5. Cv ya Elie Mpanzu Winga Mpya Simba Sc
  6. Yanga Vs CBE SA Leo 21/09/2024 Saa Ngapi
  7. Mo afanya Umafia Dar, Amshusha Mpanzu usiku
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo