Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo SUA

Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) | Tangazo La Ajira Za Muda 2000 Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo | Ajira Za Muda 2000 SUA 2024 Kupitia Programu ya Zao la Pamba

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimetangaza nafasi mpya 2000 za ajira za muda kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo. Ajira hizi zinapatikana kupitia programu maalum inayolenga kuendeleza zao la pamba nchini, ikiwa ni sehemu ya mpango mkubwa wa Building a Better Tomorrow (BBT), ambao unalenga kukuza kilimo na ajira kwa vijana na wanawake ifikapo mwaka 2030.

Mpango huu unatekelezwa kupitia mikakati mbalimbali ya kuongeza thamani katika mnyororo wa kilimo, na lengo kuu ni kusaidia wakulima wa pamba kuboresha ujuzi wao na tija.

Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimetangaza nafasi 2000 leo septemba 19 2024 kwa wahitimu wa fani za kilimo, ili kutoa huduma za ugani kwenye zao la pamba kupitia ajira za muda. Nafasi hizi zinagawanywa katika makundi mawili kama ifuatavyo:

Nafasi za Kazi Afisa Kilimo SUA (Nafasi 1000)

Majukumu ya afisa kilimo yanajumuisha kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima wa pamba, kufuatilia na kusimamia kanuni za kilimo bora, kuandaa mashamba ya mfano, kusajili wakulima, pamoja na kutoa elimu ya ubora wa zao la pamba. Afisa kilimo pia atahusika na kuratibu utoaji wa pembejeo na usimamizi wa uzalishaji katika maeneo yao.

Sifa zinazohitajika Kwa Nafasi za Kazi za Afisa Kilimo

  • Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu shahada katika fani ya sayansi ya kilimo, Agronomia au uzalishaji
  • mazao kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama
  • itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa
    kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi
    (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada

Afisa Kilimo Msaidizi (Nafasi 1000)

Afisa kilimo msaidizi atahusika na majukumu yanayofanana na yale ya afisa kilimo lakini kwa ngazi ya utekelezaji wa shamba. Majukumu yake ni pamoja na kusimamia vikundi vya wakulima, kutoa taarifa za maendeleo, na kuhakikisha kuwa wakulima wanapata pembejeo kwa wakati. Pia, atasaidia katika kuanzisha mashamba darasa na kutoa mafunzo ya vitendo kwa wakulima.

Sifa zinazohitajika Kwa Nafasi za Afisa Kilimo Msaidizi (Nafasi 1000)

  • Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu stashahada katika fani ya sayansi ya kilimo au uzalishaji mazao kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada

Faida za Ajira Hizi

Waajiriwa watafanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi itakayowekwa wazi kwenye mkataba. Hii ni fursa kubwa kwa vijana wahitimu ambao wanataka kujenga uzoefu katika sekta ya kilimo na kusaidia kuboresha kilimo cha pamba nchini. Aidha, nafasi hizi zinatoa nafasi kwa wahitimu wa mafunzo ya vitendo kuongeza ujuzi wao wa kitaalam.

Jinsi ya Kutuma Maombi Nafasi Mpya za Kazi za Muda Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

Waombaji wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Rasi wa Ndaki ya Kilimo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kupitia barua pepe coahr@sua.ac.tz, na nakala kwa Mkurugenzi wa Shahada za Awali kupitia dus@sua.ac.tz. Maombi yanapaswa kuambatanishwa na:

  • Nakala za vyeti vya kuzaliwa, NIDA, vyeti vya elimu na vyeti vya taaluma.
  • Wasifu wa mwombaji (CV).
  • Picha mbili za pasipoti za hivi karibuni.

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 25 Septemba 2024.

Bofya Hapa Kupakua Tangazo La Ajira Za Muda 2000 Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Nafasi Mpya za Kazi Ajira Portal September 2024
  2. Taarifa Muhimu kwa Waombaji Kazi za Ualimu AJira Portal 14 September 2024
  3. Kuhakiki Mwajiri Ajira Portal (Employer Confirmation): Mwongozo Kamili kwa Walimu
  4. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal 2024
  5. Nafasi Mpya za Kazi Air Tanzania (ATCL) September 2024
  6. Nafasi Mpya za Kazi Benki ya NMB September 2024
  7. Nafasi za Kazi Wizara ya Ardhi 2024 (Ajira ya Muda Mfupi)
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo