Viwango Vipya vya Posho Serikalini 2024

Viwango Vipya vya Posho Serikalini 2024 | Viwango vya Posho kwa Watumishi wa Umma

Serikali ya Tanzania imefanya marekebisho makubwa katika viwango vya posho za wafanyakazi wa umma kwa mwaka 2024.

Viwango hivi vipya vya posho kwa watumishi wa Umma vimepokelewa kwa shangwe na wadau mbalimbali kwa kuwa hatua hii inaongeza mzunguko wa fedha mitaani, na kuboresha hali ya maisha ya wafanyakazi wa umma.

Marekebisho haya ni sehemu ya jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wafanyakazi wanapata motisha ya kufanya kazi kwa bidii huku wakipata stahiki zinazokidhi gharama za maisha ya sasa. Katika mabadiliko hayo, viwango vya posho za safari na kazi maalum vimeongezeka, na hapa chini tunachambua kwa kina kuhusu viwango hivyo vipya.

Viwango Vipya vya Posho Serikalini 2024

Viwango Vipya vya Posho Serikalini 2024

Serikali ya Tanzania ilitangaza ongezeko kubwa la viwango vya posho kwa watumishi wa umma kuanzia mwaka 2022. Hatua hii ililenga kuboresha maslahi ya watumishi na kutambua mchango wao katika ujenzi wa taifa. Miongoni mwa posho zilizopanda ni pamoja na posho ya kujikimu na posho ya kazi maalumu.

Hapa, Habariforum tutaangazia kwa undani mabadiliko haya, athari zake kwa watumishi na uchumi kwa ujumla, pamoja na taarifa kamili kuhusu viwango vipya vya posho serikalini. Pia, yatafafanua baadhi ya posho nyingine muhimu zinazotolewa kwa watumishi wa umma na umuhimu wake katika utekelezaji wa majukumu yao.

1. Posho za Kujikimu Safari

Kuanzia Julai 2022, posho za kujikimu kwa wafanyakazi wa umma wanaosafiri kikazi zimepanda. Kwa sasa, kiwango cha juu cha posho za safari ni Shilingi 250,000, kutoka Sh120,000, huku kiwango cha chini kikifikia Shilingi 100,000, kutoka Sh80,000. Ongezeko hili ni ishara ya kutambua changamoto za gharama za maisha zinazowakabili wafanyakazi wanapokuwa safarini.

2. Posho kwa Kazi Maalum

Wafanyakazi wa umma wanaofanya kazi maalum nao wamepata ongezeko la posho. Viwango hivi sasa ni kama ifuatavyo:

  • Ngazi ya chini: Kutoka Sh15,000 hadi Sh30,000 kwa siku.
  • Ngazi ya kati: Kutoka Sh20,000 hadi Sh40,000 kwa siku.
  • Ngazi ya juu: Kubaki katika kiwango cha Sh30,000 kwa siku.

Marekebisho haya yameongeza hamasa kwa wafanyakazi kufanya kazi kwa bidii, kwani wanajua kuwa kazi maalum zitawapatia kipato cha ziada cha kuendesha maisha yao.

3. Posho za Vikao (Sitting Allowance)

Wafanyakazi wanaoshiriki kwenye vikao vya kitaifa kama vile bodi, kamati maalum, na kamati za wafanyakazi watapokea posho za vikao kulingana na Waraka wa Utumishi wa Serikali Na.2 wa mwaka 2010. Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umedhibitisha kuwa posho hizi zitalipwa kwa vikao maalum vilivyoidhinishwa na mamlaka husika, huku akisisitiza kwamba vikao vya kawaida havitastahili posho isipokuwa kwa ruhusa maalum kutoka kwa Mtendaji Mkuu.

4. Posho ya Chakula (Lunch Allowance)

Serikali pia imeimarisha viwango vya posho ya chakula kwa watumishi wa umma, ambapo kwa sasa kiwango cha juu ni Shilingi 200,000 kwa mwezi kwa mtumishi, kutegemea na uwezo wa kituo husika cha kazi katika uzalishaji na ukusanyaji wa mapato. Kituo ambacho hakijafikia kiwango hiki bado kinaweza kuomba ruhusa kuongeza kiwango kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa taasisi husika.

5. Posho ya Usafiri

Wafanyakazi wa umma wa kudumu na wa mkataba, ambao hawatumii magari ya ofisi, watalipwa posho ya usafiri ya Shilingi 80,000 kwa mwezi. Hii itasaidia kupunguza mzigo wa gharama za usafiri kwa wafanyakazi hao wanapokwenda kazini kila siku.

6. Posho ya Masaa ya Ziada (Extraduty Allowance)

Serikali imeweka viwango maalum vya posho kwa wafanyakazi wanaofanya kazi za ziada. Posho ya masaa ya ziada italipwa kulingana na kazi zilizopo, lakini imewekwa ukomo wa idadi ya siku ambazo mtumishi anaruhusiwa kufanya kazi za ziada kwa mwezi:

  • Wasaidizi wa ofisi, madereva na watumishi wa chini: Siku zisizozidi 10 kwa mwezi.
  • Maofisa na Mameneja: Siku zisizozidi 5 kwa mwezi.

7. Posho ya Safari

Kwa watumishi wa umma wanaosafiri kikazi, viwango vya posho za safari vimeidhinishwa kulingana na sheria na taratibu zilizopo. Wafanyakazi hao wanatakiwa kusimamia matumizi bora ya bajeti ya safari ili kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao bila kutumia fedha nyingi zisizo na tija.

8. Posho ya Kuosha Magari

Kwa madereva wa magari ya ofisi za wizara Ya Ujenzi Na Uchukuzi Wakala Wa Ufundi Na Umeme Tanzania (TEMESA), Serikali imelipa posho ya kuosha magari kwa mwezi ili kuhakikisha magari yanakuwa safi wakati wote. Kiwango hiki kimewekwa kuwa:

  • Dereva wa Mtendaji Mkuu na wa magari ya Coaster: Tshs 80,000 kwa mwezi.
  • Madereva wengine: Tshs 60,000 kwa mwezi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Viwango vya Posho kwa Watumishi wa Umma, unaweza kutembelea:

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Majina ya Walioitwa kwenye Usaili Ajira Portal 2024
  2. Mwisho Wa Kutuma Maombi Ya Mkopo HESLB 2024/2025
  3. Mfano wa Barua ya Kuomba Kazi Ajira Portal
  4. Nafasi Mpya Za Kazi MDAs NA LGAs Agosti 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo