Msimamo wa Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025 | Msimamo wa Kundi H Kufuzu AFCON 2025 | Msimamo wa Kundi la Taifa Stars
Katika mbio za kufuzu AFCON 2025, Tanzania ipo kwenye Kundi H pamoja na timu za DR Congo, Guinea, na Ethiopia. Hili ni kundi lenye changamoto kubwa kwani lina timu zenye uzoefu wa kimataifa na wachezaji wenye viwango vya hali ya juu.
Timu Zinazoshiriki Kundi H Michuano ya Kufuzu AFCON 2024/25
Tanzania inapambana na mataifa matatu ambayo yanashikilia nafasi tofauti katika viwango vya soka vya dunia vya FIFA. DR Congo iko juu kwa nafasi ya 60 duniani, Guinea ipo nafasi ya 77, Tanzania inakamata nafasi ya 113, na Ethiopia ndiyo inashika nafasi ya 143.
1. DR Congo
DR Congo ni timu yenye historia kubwa katika soka la Afrika, ikifahamika kwa kutoa wachezaji wengi wanaocheza ligi mbalimbali barani Ulaya na hata ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika miaka ya hivi karibuni, wachezaji wa DR Congo wamekuwa wakihamia Tanzania kucheza ligi ya ndani, akiwemo Djuma Shaban (Simba SC) na Chadrack Boka (Azam FC). Aidha, DR Congo imekuwa mpinzani wa mara kwa mara wa Taifa Stars katika michuano ya kimataifa, na mechi kati ya mataifa haya mawili huwa ni za upinzani mkali.
2. Guinea
Guinea inajivunia wachezaji wenye vipaji vikubwa, akiwemo kipa wao nyota Moussa Camara, anayekipiga Simba SC. Guinea pia ina mshambuliaji hatari, Serhou Guirassy, ambaye anacheza katika klabu ya Borussia Dortmund nchini Ujerumani. Timu hii imesajili wachezaji wengi wanaocheza ligi za Ulaya, na inatarajiwa kuwa na upinzani mkali katika kundi hili.
3. Ethiopia
Ethiopia ni timu inayoonekana kuwa na changamoto nyingi, hasa ikilinganishwa na washindani wake wa kundi H. Hata hivyo, Ethiopia inabaki kuwa mpinzani muhimu, na licha ya kutokuwa na wachezaji wengi wenye uzoefu wa kimataifa, wanaweza kutoa upinzani mkubwa kutokana na ari yao ya kusaka mafanikio.
Msimamo wa Kundi la Tanzania Kufuzu AFCON 2025
Tanzania imewahi kushiriki michuano ya AFCON mara tatu (1980, 2019, na 2024), lakini matokeo hayajawahi kuwa ya kuridhisha. Katika kila ushiriki, Taifa Stars imekuwa ikimaliza mkiani kwenye makundi yake bila ya mafanikio makubwa.
1. Ushiriki wa 1980: Mwaka 1980, Taifa Stars ilishiriki AFCON kwa mara ya kwanza nchini Nigeria, ambapo walimaliza nafasi ya mwisho katika Kundi A baada ya kukusanya pointi moja tu.
2. Ushiriki wa 2019: Baada ya miaka mingi, Tanzania ilirejea tena kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019 huko Misri, lakini haikuweza kuvuka hatua ya makundi baada ya kupoteza mechi zake zote dhidi ya Algeria, Senegal, na Kenya.
3. Ushiriki wa 2024: Mwaka 2024 nchini Ivory Coast, Taifa Stars ilifanikiwa kupata pointi mbili, lakini bado ilishindwa kufuzu hatua ya mtoano, baada ya kumaliza mkiani mwa Kundi F.
Kwa jumla, Tanzania imefanikiwa kufunga mabao sita tu katika michuano ya AFCON, huku ikiruhusu mabao 18. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa bado kuna changamoto kubwa ya ufungaji, jambo ambalo ni muhimu kurekebishwa endapo Tanzania inataka kufanikiwa zaidi kwenye michuano ya AFCON.
Mapendelezo ya Mhariri
Leave a Reply