Kikosi cha Taifa Stars Vs Ethiopia Leo September 4 2024 | Kikosi cha Taifa Stars Leo Dhidi ya Ethiopia Kufuzu AFCON 2025 | Kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania VS Ethiopia Leo
Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Tanzania, Taifa Stars, wanatarajiwa kushuka dimbani leo, Septemba 4, 2024, kukabiliana na Ethiopia katika mechi muhimu ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.
Mchezo huu unafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, kuanzia majira ya saa 1:00 usiku, na unatarajiwa kuwa mchezo wenye mvuto wa kipekee na kipimo muhimu kwa timu ya taifa ya Tanzania kuelekea michuano mikubwa ya bara la Afrika.
Benchi la ufundi la Taifa Stars likiongozwa na kocha mkuu Hemed Suleiman, limeweka wazi kuwa maandalizi ya mchezo huu yamekamilika kwa asilimia kubwa. Taifa Stars inajivunia kuwa na kikosi chenye ari kubwa na matumaini ya kufanya vizuri.
Kocha Hemed amesema kwamba licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji tegemeo kama Mbwana Samatta na Simon Msuva, timu inajiamini kwa wale waliochaguliwa kufanya kazi uwanjani.
Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Taifa Stars, alithibitisha kuwa kikosi kimepata muda wa kutosha kujiandaa, huku akibainisha kuwa maandalizi yamefikia asilimia 80.
Wachezaji wote wameonyesha nia ya kujituma na kupambana kuhakikisha wanapata ushindi muhimu katika mechi hii.
Kwa upande wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kupitia Ofisa Habari wake Cliford Ndimbo, ametoa wito kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuipa sapoti Taifa Stars katika mchezo huu muhimu. Ndimbo alisisitiza kuwa wachezaji wako tayari kwa changamoto hiyo na wanahitaji nguvu ya mashabiki kuwapa hamasa zaidi.
Kikosi cha Taifa Stars Vs Ethiopia Leo September 4, 2024
Kikosi cha Taifa Stars kinachoingia dimbani leo kinajumuisha wachezaji wenye uzoefu na vijana wenye nguvu na morari kubwa ya kuipambania bendera ya Tanzania. Licha ya kutokuwepo kwa wachezaji kama Samatta na Msuva, kocha Hemed Suleiman amewataka Watanzania kuwa na imani na kikosi hiki ambacho kimeonyesha kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya vizuri.
Edwin Balua, mmoja wa wachezaji walioitwa, ameeleza kuwa kwake ni fahari kubwa kupewa nafasi ya kuiwakilisha nchi na ameahidi kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha Taifa Stars inapata matokeo chanya. Balua alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wachezaji na mashabiki katika kipindi hiki muhimu.
Hapa Habariforum tutakuletea kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa stars kitakacho anza katika mchezo huu dhidi ya Ethiopia. Kikosi kinatarajiwa kutangazwa lisaa limoja kabla ya mchezo kuanza hivyo endelea kutembelea ukurasa huu ili kujua ni kina nani hasa watakao anza kuipambania bendera ya Tanzania katika michuano hii ya Afrika.
Historia ya Taifa Stars katika AFCON
Tanzania inawania kushiriki AFCON kwa mara ya nne baada ya kufanya hivyo mwaka 1980, 2019, na 2023.
Ushiriki wa Taifa Stars katika michuano hii umekuwa na changamoto nyingi, lakini kwa sasa kikosi hiki kimejipanga kuhakikisha kinafanya vizuri na kufikia mafanikio makubwa zaidi.
Kwa mara ya kwanza mwaka 1980, Tanzania ilishiriki AFCON nchini Nigeria ambapo haikufanya vizuri, ikimaliza mkiani mwa Kundi A.
Hata hivyo, miaka ya hivi karibuni imeonyesha ukuaji mkubwa wa timu hiyo, ikiwemo kufuzu kwa michuano ya AFCON mwaka 2019 nchini Misri na mwaka 2023 nchini Ivory Coast.
Matarajio ya Mchezo wa Leo
Mchezo wa leo ni kipimo muhimu kwa Taifa Stars. Ethiopia ni moja ya timu ambazo zimekuwa zikipewa nafasi ya kufuzu kutoka Kundi H, lakini Tanzania inatarajia kutumia faida ya kucheza nyumbani kuhakikisha wanapata ushindi. Mashabiki wanahimizwa kujitokeza kwa wingi ili kuwapa wachezaji nguvu ya ziada na kuipeleka timu yao hatua nyingine kuelekea AFCON 2025.
Kwa ujumla, Taifa Stars inahitaji kuonyesha ukomavu na uwezo wa kupambana katika kila dakika ya mchezo huu ili kuhakikisha wanaweka msingi mzuri wa safari yao ya kuelekea Morocco mwaka 2025. Ushindi katika mchezo huu utawapa Watanzania matumaini mapya na kujiandaa vyema kwa mechi zijazo.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Leo 04 September 2024
- Kocha wa Simba SC, Fadlu Davids atangazwa Kocha Bora wa mwezi Agosti
- Ratiba ya Timu ya Taifa Wasichana U17 (Serengeti Girls) UNAF Tunisia 2024
- Ratiba YA Ligi Kuu Ya Zanzibar (Pbz Premier League) 2024/2025
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
- Kikosi cha Taifa Stars Kufuzu AFCON 2025
Leave a Reply