Mbappe Avunja Ukame wa Magoli, Afunga Bao Lake La Kwanza La Liga
Kylian Mbappe, nyota mpya wa mabingwa wa Ulaya Real Madrid, hatimaye amevunja ukame wa magoli na kufunga bao lake la kwanza katika michuano ya ligi kuu la Hispania La Liga, akiiwezesha timu yake kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Betis kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Ushindi huu umepandisha Madrid hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya kuonyesha uwezo mkubwa kwenye michuano ya Kombe la UEFA Super Cup dhidi ya Atalanta, ambapo alifunga bao, Kylian Mbappe alikosa kufunga katika mechi tatu za mwanzo za La Liga akiwa na Real Madrid. Ukame huu wa magoli ulimweka kwenye shinikizo kubwa kutoka kwa vyombo vya habari vya Hispania, wakimkosoa kwa kushindwa kuonyesha makali yake kwenye ligi kuu ya nchi hiyo.
Hata hivyo, Mbappe aliitikia ukosoaji huo kwa kishindo katika mechi dhidi ya Real Betis, akifunga mabao mawili muhimu yaliyowapa Real Madrid ushindi muhimu. Bao lake la kwanza lilikuja dakika ya 67 baada ya kukosa nafasi kadhaa za kufunga. Hii ilitokana na pasi nzuri ya kisigino kutoka kwa Fede Valverde, ambapo Mbappe aliupiga mpira kwa mguu wa kushoto na kumshinda kipa wa Betis.
Dakika nane baadaye, Mbappe aliongeza bao la pili kwa mkwaju wa penalti, akimaliza rasmi ukame wake wa magoli. Alipongezwa kwa juhudi zake na alishangiliwa kwa nguvu na mashabiki wa Real Madrid alipotolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Luka Modric dakika ya 84.
Madrid Yapanda Hadi Nafasi ya Pili
Ushindi huu umekuwa muhimu sana kwa Real Madrid, kwani umewapandisha hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga, wakiwa na matumaini makubwa ya kuendelea na matokeo mazuri msimu huu. Mbappe, ambaye alisajiliwa kwa matarajio makubwa, hatimaye ameanza kuonyesha thamani yake ndani ya timu, na mashabiki wa Madrid wana matumaini makubwa kwamba ataendelea kufunga mabao zaidi na kusaidia timu yao kutwaa mataji.
Mapendekezo ya Mhariri:
- Ratiba ya Mechi za Leo Septemba 02 2024
- Azam FC Katika Mbio za Kumsajili Kocha Florent Ibenge wa Al-Hilal
- Mgunda Atajwa Kuchukua Mikoba ya Zahera Namungo
- Manuel Ugarte Apewa Jezi Namba 25 ya Man United, Jezi ya Zamani ya Jadon Sancho
- Vigogo KenGold Waeka Dau Kubwa kwa Kila Ushindi
- JKU FC Mabingwa Wa Ngao ya Jamii Zanzibar 2024
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
Leave a Reply