Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024

Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024

Klabu ya Yanga inaendelea kuvunja rekodi kwa kiwango chake cha juu cha soka, huku ikizoa mamilioni ya shilingi kupitia utaratibu wa “Goli la Mama” uliowekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Katika mzunguko wa kwanza wa hatua za awali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2024 (CAF Champions league), Yanga imefanikiwa kujikusanyia kiasi cha Shilingi milioni 50 kwa mabao 10 waliyoyafunga katika mechi mbili dhidi ya Vital’O ya Burundi.

Ushindi wa Yanga umekuja na hisia tofauti kwa mashabiki na wachezaji, kwani mbali na kusonga mbele katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, pia wamejipatia zawadi nono kutoka kwa Rais Samia.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa ugenini, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku ikipokea Shilingi milioni 20 kwa mabao hayo manne. Mechi ya pili iliyochezwa nyumbani katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, ilishuhudia Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 6-0, na hivyo kuongeza kiasi kingine cha Shilingi milioni 30 kwenye akaunti yao.

Pesa Iliyochukua Yanga Goli la Mama Klabu Bingwa 2024

Ahadi ya Rais Samia na Mafanikio ya Yanga

Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kudhihirisha dhamira yake ya kuhamasisha michezo nchini Tanzania kwa kutoa zawadi kwa kila goli linalofungwa na timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya kimataifa. Utaratibu wa “Goli la Mama” unahusisha kutoa Shilingi milioni 5 kwa kila goli linalofungwa. Katika makabidhiano ya fedha hizo mwishoni mwa wiki, Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, alisisitiza kuwa Rais Samia hana mbambamba inapofika suala la kutimiza ahadi zake kwa timu za Tanzania.

Msigwa alisema, “Mama hana mbambamba, ukifunga lazima upate zawadi yako, kama ilivyokuwa kwa Yanga ambao leo (Jumamosi) wamevuna shilingi milioni 30 kutoka kwa Rais wetu wa nchi.

Katika mechi ya kwanza walivuna milioni 20 kwa mabao manne, hivyo ukichanganya na ushindi wao wa mabao sita waliopata, timu hii itakuwa imevuna shilingi milioni 50 kutoka kwa Rais Samia, kama zawadi yao nono ya Goli la Mama.”

Utaratibu wa “Goli la Mama” umeleta hamasa kubwa kwa wachezaji wa Yanga na timu nyingine za Tanzania. Fedha zinazotolewa kwa kila goli zimeongeza ari ya ushindani na kuimarisha michezo nchini.

Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kuunga mkono michezo na kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na timu zenye ushindani katika ngazi ya kimataifa. Huu ni mfano bora wa jinsi viongozi wanaweza kushiriki moja kwa moja katika maendeleo ya michezo kwa manufaa ya taifa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Yanga Kucheza na CBE SA Ya Ethiopia Klabu Bingwa Septemba 2024
  2. Coastal Union Yatolewa Kombe la Shirikisho CAF
  3. Usajili wa Mukwala na Ahou Waanza Kulipa Msimbazi
  4. Matokeo Simba Vs Fountain Gate Leo 25/08/2024
  5. PSG Hatarini Kufungiwa Kushiriki UEFA Baada ya Mbappe Kudai €55M za Mishahara na Marupurupu
  6. Ronaldo Azindua Rasmi Chaneli ya YouTube
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo