Matokeo ya APR Vs Azam Fc Leo 24/08/2024

Matokeo ya APR Vs Azam Fc Leo 24/08/2024 | Matokeo ya APR Dhidi ya Azam leo Klabu Bingwa

Wana rambaramba Azam FC leo watakua ugenini Rwanda kuikabili APR FC katika mchezo wa marudiano wa hatua za awali za michuano ya klabu bingwa Afrika (CAF Champions League). Mchezo huu utaanza majira ya saa moja usiku katika uwanja wa Amahoro, jijini Kigali. Mchezo huu ni muhimu kwa Azam FC kwani wanatafuta nafasi ya kufuzu hatua inayofuata baada ya kupata ushindi mwembamba wa 1-0 katika mchezo wa awali uliofanyika Dar es Salaam.

Azam FC imesafiri kwa ndege maalum hadi Kigali ikiwa na msafara mkubwa wa wachezaji, benchi la ufundi, na hata mashabiki wachache walioandamana nao kutoa sapoti. Wachezaji wote wako fiti na tayari kwa mchezo huu muhimu. Kocha Youssoyuf Dabo amesisitiza umuhimu wa kucheza kwa umakini mkubwa ili kulinda ushindi wao mwembamba.

Dabo ameweka wazi kwamba mkakati wao ni kutafuta bao la mapema ili kuongeza presha kwa APR na kuwafanya wafunguke zaidi. Azam wanaamini kwamba wakifanikiwa kupata bao la mapema, wataweza kuwadhibiti wapinzani wao na hatimaye kupata ushindi.

APR, mabingwa wa Rwanda leo watacheza mbele ya mashabiki wao wenye hamasa kubwa. Watahitaji kushinda kwa tofauti ya mabao mawili ili kusonga mbele. Kocha wao amewahimiza wachezaji wake kucheza kwa kujituma na kuhakikisha wanatumia vyema nafasi watakazopata.

Matokeo ya APR Vs Azam Fc Leo 24/08/2024

APR FC 2-0 Azam Fc
Full-time

APR FC 2-0 AZAM FC

Ruboneka⚽️
Gilbert ⚽️

  • 🏆 #Klabu Bingwa Afrika CAF
  • ⚽️ APR FC VS AZAM FC
  • 📆 24.08.2024
  • 🏟 Uwanja wa Amahoro
  • 🕖 Saa Moja Usiku

Angalia Hapa Kikosi cha Azam Fc VS APR Leo 24/08/2024

Matokeo ya APR Vs Azam Fc Leo 24/08/2024

Mashabiki wa Azam FC, walioandamana na timu hiyo kwenda Kigali, wanatarajiwa kutoa hamasa kubwa kwa wachezaji wao, huku pia wapinzani wa jadi wa APR, Rayon Sports, wakitarajiwa kuunga mkono Azam katika mchezo huu.

Hii ni ishara ya jinsi mechi hii ilivyo na umuhimu mkubwa, si kwa Azam pekee, bali pia kwa mashabiki wa soka nchini Rwanda.

Katika mchezo huu, Azam FC inahitaji kuwa makini na kutumia kila nafasi wanayopata ili kuweza kusonga mbele. APR FC watakuwa na shauku ya kutumia faida ya uwanja wa nyumbani na sapoti ya mashabiki wao ili kulipa kisasi.

Licha ya changamoto hiyo, Azam FC ina kila sababu ya kuamini katika uwezo wao wa kuvuka kikwazo hiki na kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano ya CAF Champions League.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Matokeo ya Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024
  2. Kikosi cha Yanga Vs Vitalo Leo 24/08/2024
  3. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  4. Usajili wa Chelsea 2024/2025
  5. PSG Hatarini Kufungiwa Kushiriki UEFA Baada ya Mbappe Kudai €55M za Mishahara na Marupurupu
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo