Viingilio Mechi ya Yanga dhidi ya Vitalo FC 24/08/2024 Club bingwa | Bei ya Tiketi Mechi ya Yanga Vs Vital’o
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania 2023/2024, Yanga SC, wanajiandaa kumalizia kile ambacho wamekianzisha Agosti 17 katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika (CAF Champions League) ambapo walikutana na timu ya Vital’O FC kutoka Burundi na kufungua kampeni yao kwa kugawa dozi ya bao 4-0 katika mchezo huo wa kwanza.
Mchezo wa marudiano umepangwa kutimua vumbi katika dimba la Benjamin Mkapa, Temeke, Dar es Salaam, mnamo Agosti 24, 2024. Mashabiki wa soka wanaotarajia kushuhudia mechi hii wana kila sababu ya kuwa uwanjani kwani inatarajiwa kuwa mtanange wa kukata na shoka, ambapo Yanga Sc imehaidi kuandika historia mpya ya kupachika magoli katika mechi hii.
Mashabiki na wapenzi wa soka wanaotaka kushuhudia mchezo huu live uwanjani wanapaswa kuhakikisha wanapata tiketi mapema, kwani viingilio vimepangwa ili kutoa nafasi kwa kila mmoja kufurahia burudani hii.
Viingilio Mechi ya Yanga dhidi ya Vitalo FC 24/08/2024 Club bingwa
- Mzunguko 5,000
- VIP C 10,000
- VIP B 20,000
- VIP C 30,000
Mapendekezo ya Mhariri:
- Vituo Vya Kununua Tiketi Mechi ya Yanga Vs Vitalo Klabu Bingwa
- Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
- Tuzo za PFA: Timu Bora ya Ligi Kuu ya Uingereza 2023/2024 Yatajwa
- Phil Foden Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora EPL MVP
- Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
- Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
Leave a Reply