Phil Foden Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora EPL MVP

Phil Foden Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora EPL MVP

Phil Foden, kiungo mshambuliaji wa Manchester City, ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL MVP) kwa msimu wa 2023/24. Hii ni baada yakua na msimu wa kipekee uliomshuhudia akichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya klabu yake, Manchester City ambayo iliibuka mabingwa wa EPL 2023/2024.

Phil Foden Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora EPL MVP

Mchango Mkubwa wa Foden kwa Manchester City

Foden aliongoza juhudi za Manchester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kufunga mabao 19, ambayo ni kiwango chake cha juu zaidi katika msimu mmoja wa ligi. Mabao haya yalikuja na pasi za mwisho (assists) nane, ambazo zilisaidia timu yake kufanikisha malengo yake. Mbali na mabao hayo, Foden alipiga hat-trick mbili, dhidi ya Brentford na Aston Villa, ambazo zilimfanya kuwa moja ya wachezaji muhimu zaidi wa timu hiyo.

Kiwango cha Foden hakikuishia tu katika Ligi Kuu ya Uingereza, bali pia aling’ara katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Katika mechi nane alizocheza, alifunga mabao matano na kutoa pasi za mabao tatu, akiwemo goli la kipekee alilofunga katika uwanja wa Santiago Bernabeu dhidi ya Real Madrid.

Mafanikio Binafsi ya Foden

Tuzo hii ya Mchezaji Bora wa EPL MVP ni mafanikio ya pekee kwa Foden, lakini sio tuzo yake ya kwanza. Akiwa na umri wa miaka 24, Foden tayari ameshawahi kushinda Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa PFA mara mbili mfululizo, mnamo mwaka 2021 na 2022. Kwa msimu huu wa 2023/24, Foden pia alishinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari wa Soka (Football Writers’ Association Footballer of the Year).

Katika mbio za kuwania tuzo hii ya Mchezaji Bora wa EPL MVP, Foden aliwashinda wachezaji wenzake wa Manchester City, Erling Haaland na Rodri, ambao pia walikuwa na msimu mzuri. Wachezaji wengine waliokuwa kwenye orodha fupi ya waliochuana na Foden ni Martin Odegaard wa Arsenal, Cole Palmer wa Chelsea, na Ollie Watkins wa Aston Villa.

Ushindi wa Phil Foden katika tuzo hii ni ishara ya kujituma kwake na mchango wake mkubwa kwa Manchester City. Akiwa bado kijana mwenye miaka 24, Foden anaonekana kuwa na mustakabali mzuri zaidi katika soka, huku akitarajiwa kuendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa klabu yake na timu ya taifa ya Uingereza.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
  2. Msimamo NBC Premier league 2024/2025 | Ligi Kuu Bara
  3. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
  4. Ratiba Ya Mechi Za Leo 19 August 2024
  5. Matokeo ya Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Klabu Bingwa
  6. Kikosi Cha Azam Vs APR Leo 18/08/2024 Club Bingwa
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo