CECAFA: Mashabiki Wa Simba Queens Watarajie Burudani, Asema Mgunda

CECAFA: Mashabiki Wa Simba Queens Watarajie Burudani, Asema Mgunda

CECAFA: Mashabiki Wa Simba Queens Watarajie Burudani, Asema Mgunda

Kikosi cha Simba Queens kimetua salama nchini Ethiopia, kikiwa na azma ya kushiriki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake (CECAFA). Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mgunda, amewahakikishia mashabiki kuwa wachezaji wake wako tayari kupambana na kuwaletea burudani tele.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mgunda alisema kuwa wachezaji wake wanafahamu vyema matarajio ya Watanzania na wako tayari kutimiza majukumu yao ya klabu na taifa. Ameongeza kuwa wachezaji wako katika hali nzuri na morali yao iko juu, wakiahidi kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano hiyo.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa kila mechi itakuwa muhimu kwao na hawatawadharau wapinzani wao wowote. Simba Queens imepangwa katika Kundi B, ambapo itaanza kampeni yake kwa kuvaana na FAD kutoka Djibouti Jumapili hii. Kisha itakutana na Kawempe Muslim FC kutoka Uganda Agosti 20, kabla ya kumaliza mechi za hatua ya makundi dhidi ya mabingwa wa Burundi, PVP Buyenzi, Agosti 22.

Mgunda amewahimiza mashabiki wa Simba Queens kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wao na kuamini kuwa watafanya vizuri katika michuano hiyo. Timu mbili zitakazomaliza katika nafasi mbili za juu katika kila kundi zitatinga hatua ya nusu fainali, na fainali ya michuano hiyo itafanyika Agosti 29.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Vilabu Bora Afrika 2024/2025 (CAF Club Ranking)
  2. KMC na Simba Wafikia Makubaliano ya Uhamisho wa Kiungo Awesu Awesu
  3. Cv ya Leonel Ateba Mshambuliaji Mpya wa Simba 2024/2025\
  4. Ahmed Arajiga Ateuliwa na CAF Kuchezesha Mechi ya Klabu Bingwa Afrika
  5. Dirisha la usajili Tanzania 2024/2025 Kufungwa Leo Agosti 15
  6. Viingilio Mechi ya Vital O FC Vs Yanga Klabu Bingwa 17/08/2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo