Matokeo ya Simba Vs Coastal union Leo Ngao ya Jamii 11/08/2024

Kikosi Cha Simba VS Coastal union Ngao ya Jamii

Matokeo ya Simba Vs Coastal union Leo Ngao ya Jamii 11/08/2024 | Matokeo ya Simba Dhidi ya Coastal union Leo

Leo, Agosti 11, 2024, Uwanja wa Benjamin Mkapa utashuhudia mtanange wa kusisimua kati ya wekundu wa msimbazi Simba Sc na wagosi wa kaya Coastal Union katika mechi ya kuamua mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii 2024. Mechi hii inatarajiwa kuanza majira ya saa tisa alasiri, ikiwapa mashabiki wa soka burudani ya kipekee kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC.

Simba Sc, wakiwa wametoka kupoteza mchezo wa nusu fainali dhidi wapinzani wao wa jadi Yanga Sc katika nusu fainali kwa bao 1-0, watakuwa wakitafuta faraja katika mchezo huu. Bao la ushindi la Yanga lilipachikwa kimiani na Max Nzegeli katika dakika za lala salama za kipindi cha kwanza, licha ya Simba kufanya mashambulizi kadhaa. Kamati ya ulinzi ya wana wa jangwani Yanga Sc, ikiimarishwa na Bacca, ilisimama kidete na kuzuia Simba kupata bao la kusawazisha.

Coastal Union, kwa upande wao, walijikuta katika nafasi hii baada ya kupokea kipigo kikali cha mabao 5-2 kutoka kwa Azam Fc. Licha ya kipigo hicho, Coastal Union watakuwa na hamu ya kuonyesha uwezo wao na kumaliza michuano hii kwa ushindi.

Kocha Mkuu wa Simba Sc, Fadlu Davids, amesisitiza umuhimu wa kushinda mchezo huu kama sehemu ya maandalizi kuelekea mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United. Amekiri ugumu wa mchezo kutokana na ubora wa Coastal Union, lakini ameonyesha imani katika kikosi chake kupata ushindi. Hussein Kazi, mlinzi wa kati wa Simba, amekiri kwamba kucheza mechi ya mshindi wa tatu haikuwa katika malengo yao, lakini wamejipanga kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi.

Matokeo ya Simba Vs Coastal union Leo Ngao ya Jamii 11/08/2024

Simba 1-0 FT Coastal union
  • Mchezo umeanza ,Dakika ya 06 Simba 0-0 Coastal Union
  • Dakika ya 10 Saleh Karabaka anaitanguliza Simba
  • Dakika ya 29 Simba 1-0 Coastal Union
  • Mapumziko; Simba 1-0 Coastal Union
  • Simba 1-0 Coastal Union FT

Angalia Hapa Kikosi Cha Simba VS Coastal union Ngao ya Jamii 11/08/2024

🏆 #Ngao Ya Jamii🇹🇿
⚽️ Simba Sc🇹🇿🆚Coastal Union FC🇹🇿
📆 11.08.2024
🏟 Uwanja wa Benjamin Mkapa
🕖 Saa Tisa Alasiri🇹🇿

Matokeo ya Simba Vs Coastal union Leo Ngao ya Jamii 11/08/2024

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wwenye mvuto wa kipekee, huku timu zote zikiwa na hamu ya kumaliza michuano kwa ushindi. Mashabiki wa soka wanaweza kutarajia burudani ya hali ya juu na soka la kuvutia kutoka kwa timu zote mbili. Je, Simba Sc wataweza kujikomboa na kupata ushindi, au Coastal Union watashangaza wengi na kuibuka washindi? Jibu litapatikana kesho katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Waamuzi Watakao chezesha Simba SC vs Coastal Union Ngao ya Jamii 2024: Hawa Hapa!
  2. Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2024/2025 (NBC Premier league)
  3. Viingilio Mechi ya Fainali ya Yanga Vs Azam Fc Ngao Ya Jamii 2024
  4. Ratiba ya Fainali Ngao Ya Jamii 2024
  5. Matokeo ya Yanga Vs Simba Leo Ngao Ya Jamii 08/08/2024
  6. Matokeo ya Azam Vs Coastal Union Leo Ngao ya Jamii 08/08/2024
  7. Matokeo ya Ngao ya Jamii 2024
  8. Washindi wa Ngao ya Jamii Miaka Yote
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo