Khalid Aucho Atwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Yanga
Baada ya kukosekana katika tuzo za TFF Katika msimu wa 2023/24, Khalid Aucho amepewa heshima kwa kutangazwa kua mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Yanga. Tuzo hii inatambua mchango mkubwa wa Aucho ndani na nje ya uwanja, akiwavutia mashabiki na kuonyesha uwezo wa hali ya juu katika kila mchezo.
Khalid Aucho alionyesha kiwango bora katika safu ya kiungo wa Yanga. Kwa umahiri wake wa kupokonya mipira, kupiga pasi sahihi, na kuimarisha ulinzi, Aucho amekuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Yanga. Katika msimu uliopita wa 2023/2024, alikuwa na ushirikiano mzuri na wachezaji wenzake, akihakikisha Yanga inapata matokeo mazuri.
Shukrani za Khalid Aucho kwa Mashabiki
Wakati wa kukabidhiwa tuzo, Aucho alitoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wa Yanga kwa sapoti yao isiyo na kifani. Aliandika kwenye mitandao ya kijamii, “Tuzo hii isingewezekana bila usaidizi, uaminifu wenu usioyumbayumba na upendo wa dhati. Mashabiki wa Yanga asante kwa kuwa mwamba wangu. Upendo mwingi na heshima. Tuna mengi ya kufanya msimu huu.”
This award wouldn’t be possible without your unwavering support, trust and love. @YoungAfricansSC fans thank you for being my rock. Much love and respect. We have much to do this season.🙏🔰🔰 pic.twitter.com/HAVDJoUqhZ
— Aucho Khalid🇺🇬 (@aucho_khalid08) August 5, 2024
Mapendekezo ya Mhariri:
- Viingilio Yanga Vs Simba Vita ya Ngao Ya Jamii 2024
- Ratiba ya Ngao ya Jamii 2024
- Wiki ya Mwananchi 2024 (Yanga Day): Tarehe, Matukio na Bei ya Tiketi
- Kikosi Cha Simba 2024/2025 | Wachezaji Wote wa Simba
- Orodha ya Makocha Timu za Ligi Kuu ya NBC 2024/2025
- Kibu Denis Arejea Simba SC Huku Akisubiri Uamuzi wa Kamati ya Nidhamu
- Meddie Kagere Aongezewa Mkataba Wa Mwaka Mmoja Namungo FC
- Washindi wa Tuzo za TFF 2023/2024
Leave a Reply