Mshindi wa MVP Ligi Kuu Tanzania Bara NBC 2023/2024 Amepatikana
Usiku wa tarehe 1 Agosti, 2024, ulikuwa wa kihistoria kwa kiungo mshambuliaji wa Young Africans (Yanga), Stephane Aziz Ki.
Katika hafla iliyofana kwenye ukumbi wa Super Dome, Masaki jijini Dar es Salaam, Aziz Ki aliibuka mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka (MVP) wa Ligi Kuu Tanzania Bara NBC msimu wa 2023/2024.
Aziz Ki alipokea tuzo yake ya MVP kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo na Utamaduni, Gerson Msigwa, aliyekuwa ameambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas.
“Nina furaha kubwa kushinda tuzo hii. Hii ni kwa ajili ya wachezaji wenzangu, mashabiki, wanachama, na uongozi,” alisema Aziz Ki kwa furaha, akiwa ameandamana na mwanamitindo Hamisa Mobeto kwenye jukwaa.
“Nawataka mashabiki wa Yanga wajitokeze kutuunga mkono katika mechi zote ili tuendelee kupata kujiamini na kung’ara katika mashindano yote,” aliongeza.
Tuzo Nyengine Alizobeba Stephane Aziz Ki
Mbali na kutajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka, Aziz Ki alishinda tuzo tatu nyingine katika usiku huo wa tuzo. Aliibuka mshindi wa kiatu cha dhahabu kwa kufunga mabao 21, akimshinda mpinzani wake wa karibu Feisal “Fei Toto” Salum wa Azam FC aliyefunga mabao 19.
Aziz Ki pia alitunukiwa tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho la CRDB. Fei Toto alitajwa kuwa mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho la CRDB.
Haya ni mafanikio makubwa kwa mchezaji huyu kutoka Burkina Faso, ambaye alijiunga na Yanga kwa mara ya kwanza katika msimu wa 2022/2023.
Yanga SC Yatamba Katika Tuzo
Hafla hiyo haikuwa ya Aziz Ki pekee. Yanga SC iliwakilishwa vyema baada ya wachezaji wake wengi kushinda tuzo nyingi, ikiwemo:
- Mlinzi Bora: Ibrahim “Bacca” Hamad wa Yanga.
- Kikosi Bora cha Ligi: Wachezaji watano wa Yanga (Yao Kouassi, Dickson Job, Ibrahim “Bacca” Hamad, Mudathir Yahya, and Maxi
- Nzengeli) waliingia kwenye kikosi bora.
- Mfungaji Bora wa ASFC: Clement Mzize wa Yanga.
- Kipa Bora wa ASFC: Djigui Diara wa Yanga.
- Kocha Bora wa Ligi: Miguel Gamondi wa Yanga.
Hitimisho
Mafanikio haya ya Aziz Ki yanaashiria mchango mkubwa aliouleta katika timu ya Yanga na mpira wa miguu nchini Tanzania. Tuzo hizi zinaonyesha jitihada zake binafsi na mchango wa timu kwa ujumla. Wakati Yanga ikijiandaa kwa msimu mpya, mashabiki wana matumaini makubwa ya kuendelea kuona mafanikio zaidi kutoka kwa Aziz Ki na wachezaji wenzake.
Kwa taarifa zaidi, Soma hapa kujua washindi wote wa Tuzo ya Shirikiho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) 2023/2024
Leave a Reply