Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money

Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money | Namna ya kulipia Tiketi za Mpira kwa Airtel Money

Kama wewe ni shabiki wa soka basi bila shaka unaeza kuwa na uelewa wa vibe na furaha inayopatikana kwa kuweza kushuhudia timu yako pendwa ikicheza mechi ukiwa uwanjani. Ili kuweza kutazama mechi zozote za mpira, kununua tiketi ni moja ya zoezi ambalo kila shabiki anapaswa kukamilisha kabla ya kuruhusiwa kuingia uwanjani. Hapa tumekuletea muongozo kamili wa jinsi ya kununua tiketi za mpira kwa kutumia huduma ya Airtel Money.

Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money

Jinsi ya Kununua Tiketi za Mpira Airtel Money

Zifuatazo ni hatua za Kununua Tiketi za Mpira kwa Airtel Money

Piga *150*60#

Anza kwa kupiga *150*60# kwenye simu yako. Hii itakupeleka moja kwa moja kwenye menyu ya Airtel Money.

Chagua 5 > Lipa Bill

Baada ya kuingia kwenye menyu ya Airtel Money, chagua namba 5 ambayo ni “Lipa Bill”.

Chagua # > Next

Chagua # ili kuendelea na hatua inayofuata.

Chagua 8 > Malipo Mtandao

Kwenye menyu inayofuata, chagua namba 8 ambayo ni “Malipo Mtandao”.

Chagua 1 > Tiketi za Michezo

Chagua namba 1 kwenye menyu ya “Tiketi za Michezo”.

Chagua 1 > Football Tickets

Baada ya hapo, chagua namba 1 kwa “Football Tickets”.

Chagua Mechi Unayotaka Kulipia

Kwenye orodha ya mechi zinazopatikana, chagua mechi unayotaka kulipia tiketi.

Chagua Aina ya Tiketi Unayotaka Kulipia

Baada ya kuchagua mechi, utaulizwa uchague aina ya tiketi unayotaka kulipia.

Weka Namba ya Kadi yako ya (N-Card)

Weka namba ya kadi yako ya N-Card ili kukamilisha mchakato wa malipo.

Ingiza Namba ya Siri

Ingiza namba yako ya siri ya Airtel Money ili kuthibitisha malipo.

Thibitisha

Hatua ya mwisho ni kuthibitisha malipo yako. Utapokea ujumbe wa kuthibitisha kuwa malipo yako yamekamilika na tiketi yako imekatwa.

Faida za Kununua Tiketi kwa Kutumia Airtel Money

  1. Urahisi na Uharaka: Ununuzi wa tiketi kwa kutumia Airtel Money ni rahisi na wa haraka. Huna haja ya kwenda kwenye vituo vya kuuza tiketi au kusimama kwenye foleni ndefu.
  2. Usalama: Malipo ya mtandaoni kupitia Airtel Money ni salama. Hutakiwi kubeba fedha taslimu ambazo zinaweza kupotea au kuibiwa.
  3. Inapatikana Wakati Wowote: Unaweza kununua tiketi zako wakati wowote na mahali popote, mradi tu unayo simu na salio la kutosha kwenye akaunti yako ya Airtel Money.
  4. Msaada kwa Wateja: Airtel Money ina huduma nzuri ya msaada kwa wateja ambayo inaweza kukusaidia endapo utakutana na changamoto yoyote wakati wa kununua tiketi.

Mapendekezo ya Mhariri:

  1. Mfano wa Barua ya Maombi ya Kazi ya Mtendaji wa Kijiji na Mtaa
  2. Mfano wa Barua za Kazi ya Ualimu TAMISEMI 2024
  3. Jinsi ya Kupata Namba ya NIDA Kwa SMS
  4. Jinsi ya Kupata Cheti cha Kuzaliwa Kwa Mtu Mzima
  5. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)
  6. Jinsi Ya Kuangalia Matokeo Ya Kidato Cha Sita 2024
  7. Jinsi ya Kujiunga na Mfumo wa Maombi ya Ajira TAMISEMI
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo