Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II TAMISEMI 2024: Wauguzi 2282 Wahitaji
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa imetangaza kukaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenyesifa na uwezo wa kujaza nafasi 2282 katika fani ya Muuguzi. Nafasi hizi za kazi ni kutoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Mkoa Wa Arusha 65, Dar Es Salaam 96, Dodoma 133, Geita 90, Iringa 68, Kagera 125, Katavi 51, Kigoma 85, Kilimanjaro 65, Lindi 109, Manyara 125, Mara 95, Mbeya 83, Morogoro 71, Mtwara 155, Mwanza 89, Njombe 48, Pwani 86, Rukwa 52, Ruvuma 72, Shinyanga 77, Simiyu 72, Singida 116, Songwe 58, Tabora 79 Na Tanga 117.
Majukumu Ya Kazi Muuguzi II (Nurse II)
- Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya;
- Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi;
- Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi;
- Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani;
- Kutoa ushauri nasaha;
- Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango;
- Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto;
- Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya;
- Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi; na
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
Sifa Za Mwombaji Nafasi Mpya Za Ajira Muuguzi II (Nurse II)
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.
Ngazi Ya Mshahara
Kwa kuzingatia Ngazi ya Mshahara ya Serikali TGHS A
Masharti Ya Jumla Kwa Waombaji wa Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini serikalini;
Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma;
Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/Wakili.
Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombiya nafasi za kazikwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina yawadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kuzaliwa, kidato cha Nne, kidato cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho, na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- – Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- – Computer Certificate
- – Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
“Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo zakidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 20 Julai, 2024
MUHIMU: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamojana vyeti vya elimu, anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
- KATIBU,
- OFISI YA RAIS,
- SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA,
- L. P. 2320, DODOMA.
Jinsi Ya Kutuma Maombi Nafasi Mpya za Ajira Muuguzi II
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira(Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;http://portal.ajira.go.tz (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa‘Recruitment Portal’)
Mapendekezo ya Mhariri:
Leave a Reply