Alama za Ufaulu Kidato cha Sita 2024

Viwango vya ufaulu

Alama za Ufaulu Kidato cha Sita 2024 (Madaraja ya ufaulu kidato cha Sita)

Mitihani ya Taifa ya kidato cha sita ni moja ya mitihani muhimu sana katika safari ya elimu nchini Tanzania. Mtihani huu hufanywa na wahitimu wa kidato cha sita kwa ajili ya kuhitimisha masomo ya miaka miwili ya elimu ya sekondari katika ngazi ya A-level. Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ndilo lenye jukumu la kusimamia na kuendesha zoezi la ufanyikaji wa mtihani huu, pamoja na mitihani ya darasa la saba na kidato cha nne ambayo yote hufanywa na shule zote nchini Tanzaia.

Mtihani wa kidato cha sita ni muhimu katika mtaala wa elimu nchini Tanzania kwa sababu ndio mtihani ambao hutumika kama kigezo cha wanafunzi kujiunga na vyuo vya elimu ya juu kama vile vyuo vya shahada na stashahada. Vilevile, makampuni mbalimbali hutumia matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kama kigezo cha kuajiri wafanyakazi katika nyanja mbalimbali. Hapa tumekuletea alama za ufaulu wa kidato cha sita 2024, pamoja na madaraja ya ufaulu kidato cha sita.

Alama za Ufaulu Kidato cha Sita 2024

Uchakataji wa matokeo ya Upimaji wa Kidato cha Sita umezingatia viwango vya alama , madaraja ya ufaulu na utaratibu wa matumizi ya alama endelevu (CA) kama ifuatavyo

Gredi Alama Uzito Wa Gredi (Pointi) Maelezo
A 80-100 1 Excelent
B 70-79 2 Very Good
C 60-69 3 Good
D 50-59 4 Average
E 40-49 5 Satisfactory
S 35-39 6 Subsidiary
F 0-34 7 Fail

Madaraja ya ufaulu kidato cha Sita

Mfumo wa madaraja ya ufaulu kwa mtihani wa kidato cha sita unabainishwa kwa kutumia mbinu mbili:

  1. Jumla ya Alama (Total Point Grading System)
  2. Divisheni.

Katika mfumo wa Jumla ya Alama, kila somo litakuwa na uzito maalum kulingana na ugumu na umuhimu wake. Alama za mwanafunzi katika kila somo zitazidishwa na uzito wa somo husika, na jumla ya alama hizo zitaamua daraja la mwanafunzi.

Mfumo wa Divisheni unajumuisha kugawa wanafunzi katika makundi (divisions) kulingana na ufaulu wao wa jumla. Kila kundi litawakilisha kiwango fulani cha ufaulu, na wanafunzi watapangwa katika kundi husika kulingana na alama zao. Mbinu hizi mbili hutumika kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa ufaulu wa mwanafunzi unapimwa kwa usahihi na kwa kuzingatia vigezo mbalimbali.

Watahiniwa waliofanya masomo matatu ya tahasusi au zaidi watapata Daraja la I, II, III, au IV kulingana na jumla ya alama zao.

Watahiniwa waliofanya chini ya masomo matatu ya tahasusi watafaulu kwa daraja la IV ikiwa watafaulu angalau masomo mawili katika Gredi S au somo moja katika Gredi A, B, C, D, au E.

Jedwali lifuatalo linaonesha Madaraja  ya ufaulu kidato cha sita yanayotumiwa na baraza la mitihani Tanzania (NECTA)

Daraja ACSEE (K6) Maelezo
I 3-9 Bora sana (Excellent)
II 10-12 Vizuri sana (Very Good)
III 13-17 Vizuri (Good)
IV 18-19 Inaridhisha (Satisfactory)
0 20-21 Feli (Fail)

Alama za Ufaulu Kidato cha Sita 2024

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Usajili Watainiwa Kidato Cha Sita 2025 Kuanzia 01 Julai 2024
  2. Matokeo ya kidato cha sita 2024 Yanatoka Lini?
  3. Mwisho Wa Kutuma Maombi Ya Mkopo HESLB 2024/2025
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo