Majina ya Wachezaji Wapya Simba 2024/2025

Majina ya Wachezaji Wapya Simba 2024/2025 | Majina ya wachezaji wapya Simba Simba | wachezaji wapya simba

Msimu wa 2023/2024 ulikuwa ni msimu wa huzuni na majonzi kwa mashabiki wa wekundu wa msimbazi, Simba SC. Timu yao ilikosa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC na hata nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAF, baada ya kumaliza msimu katika nafasi ya tatu. Simba SC ilimaliza msimu ikiwa na jumla ya pointi 69, sawa na Azam FC waliomaliza katika nafasi ya pili, lakini Azam waliongoza kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.

Katika michuano ya ndani, Simba SC haikuweza kufikia malengo yake, na hali ilikuwa mbaya zaidi katika mashindano ya CAF. Simba SC ilishindwa kutamba na ikaondolewa tena katika hatua ya robo fainali, hali iliyopelekea wapinzani wao kuwadhihaki kwa jina la “Mwakarobo.”

Katika jitihada za kuimarisha kikosi kuelekea msimu wa 2024/2025, uongozi wa Simba SC umefanya mabadiliko makubwa. Baadhi ya wachezaji waliokuwa na viwango hafifu wameachwa na nyota wapya wameletwa ili kuimarisha timu. Lengo ni kuhakikisha Simba SC inarejea kwenye ushindani na kufikia malengo makubwa, ikiwemo kushinda Ligi Kuu ya NBC na kufanya vizuri katika michuano ya CAF.

Kwa mashabiki wa Simba SC, matumaini ni makubwa kwa nyota wapya waliojiunga na timu. Uongozi unaamini kwamba maboresho haya yatakuwa na matokeo chanya na kuleta furaha kwa mashabiki ambao wamekuwa na kiu ya mafanikio. Kila hatua imechukuliwa kwa umakini kuhakikisha Simba SC inarudi kwenye kiwango chake bora na kushindania mataji makubwa msimu ujao.

Wachezaji Wapya Simba 2024/2025

1. Lameck Lawi

Wachezaji Wapya Simba 2024/2025

 

Klabu ya Simba imechukua hatua ya kwanza katika kuimarisha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili beki chipukizi Lameck Elius Lawi. Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 18 ametia saini mkataba wa miaka mitatu, ukiwa na kipengele cha kuongezwa mwaka mmoja zaidi, akitokea Coastal Union ya Tanga.

Lawi, licha ya umri wake mdogo, amejipatia sifa kama mmoja wa walinzi bora chipukizi nchini, akiwa ameonyesha kiwango cha juu akiwa na Coastal Union msimu uliopita. Uwezo wake wa kucheza mipira ya juu, kukaba kwa utulivu, na kuanzisha mashambulizi kutoka nyuma umeibua hamu kubwa kutoka kwa Simba.

Usajili huu unadhihirisha dhamira ya Simba ya kujenga kikosi kipya chenye ushindani mkubwa katika msimu ujao. Lawi anatarajiwa kuongeza nguvu na ubora katika safu ya ulinzi ya Simba, akiwa na uwezo wa kucheza kama beki wa kati. Urefu wake na uwezo wa kuhimili presha unamfanya kuwa mchezaji muhimu katika kukabiliana na washambuliaji hatari wa timu pinzani.

2. Ahoua Jean Charles

Klabu ya Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Ahoua Jean Charles raia wa Ivory Coast 🇨🇮 kwa mkataba wa miaka miwili. Ahoua kinda fundi wa boli mtoto wa afu mbili mwenye umri wa miaka 22 ametokea Stella Club d’Adjamé ya nchini kwao Ivory Coast huku akiwa ndiye MVP wa msimu wa 2023/2024.

Katika msimu wa 2023/24, Ahoua ameibuka kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MVP) na klabu yake, huku akifunga mabao 12 na kutoa ‘assist’ tisa. Kiungo huyu mshambuliaji anasifika kwa kufunga mabao mengi nje ya box, kuchezesha timu, pamoja na kutengeneza nafasi kwa wenzie.

Mashabiki wengi wa simba wanategemea mambo makubwa kutoka kwa Ahoua kwa kushirikiana na nyota wengine ambao wameshasajiliwa pamoja na wale waliokuwepo kikosini. Kuelekea msimu wa Ligi 2024/25, Klabu ya Simba imekuja na utaratibu mpya kwenye usajili wa kuingiza wachezaji bora wenye uwezo na umri mdogo ili kujenga timu imara ya muda mrefu.

3. Steven Mukwala

Steven Mukwala

Klabu ya Simba SC imethibitisha rasmi Julai 2 kumsajili Steven Mukwala kutoka Klabu ya Asante Kotoko ya Nchini Ghana.

Huu ni usajili wa tatu kufanywa na Simba SC baada ya ule wa Lameck Lawi na Joshua Mutale ambao wanatarajiwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Simba kuelekea msimu wa 2024/2025.

Steven Mukwala, ambaye ni mshambuliaji mahiri na mwenye kipaji kikubwa cha kusakata boli, anatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika safu ya ushambuliaji ya Simba SC ambayo ilionekana kuwa butu msimu wa 2023/2024.

Usajili huu unakuja wakati ambapo Simba SC inajiandaa kwa msimu mpya wa ligi na michuano ya kimataifa ya CAF confederation cup, huku ikilenga kuimarisha kikosi chake na kuhakikisha mafanikio makubwa. Mukwala, mwenye uzoefu mkubwa katika ligi mbalimbali, anatarajiwa kuwa mchezaji muhimu na tegemeo katika safari ya Simba SC kuelekea ubingwa.

4. Joshua Mutale

Joshua Mutale

Joshua Mutale ni mmoja kati ya wachezaji mahiri ambao wametambulishwa kujiunga na klabu ya Simba Sc ambayo kwa sasa ipo katika uboreshaji wa kikosi chake kuelekea msimu wa 2024/2025. Mutare ni mchezaji wa pili kutambulishwa baada ya Lawi ambae alitambulishwa tarehe 20 juni 2024.

Joshua Mutale ana umri wa miaka 22 na ana uwezo wa kucheza nafasi nyingi uwanjani kwa ufanisi wa hali ya juu, Joshua anaweza kumudu nafasi ya winga ya kulia, kushoto, na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji, yaani namba 10. Akiwa na timu ya Power Dynamos msimu uliopita, Mutale alifanikiwa kufunga mabao matano na kuisaidia timu yake kupata mengine matatu katika michezo 26.

5. Abdulrazak Hamza

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kumsajili Abdulrazak Hamza, beki mahiri wa Kitanzania kutoka klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Hamza, ambaye pia amewahi kucheza katika klabu za Mbeya City, KMC FC, na Namungo FC, ametangazwa kujiunga na kikosi cha Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Usajili wake unaongeza nguvu mpya kwenye safu ya ulinzi ya Simba, ikizingatiwa ujuzi na uzoefu wake wa kucheza katika ligi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Abdulrazak Hamza

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kumsajili Abdulrazak Hamza, beki mahiri wa Kitanzania kutoka klabu ya SuperSport United ya Afrika Kusini inayoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini. Hamza, ambaye pia amewahi kucheza katika klabu za Mbeya City, KMC FC, na Namungo FC, ametangazwa kujiunga na kikosi cha Simba baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili. Usajili wake unaongeza nguvu mpya kwenye safu ya ulinzi ya Simba, ikizingatiwa ujuzi na uzoefu wake wa kucheza katika ligi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

6. Debora Fernandes

Klabu ya Simba SC imetangaza kumsajili kiungo wa kati Debora Fernandes Mavambo kutoka Mutondo Stars ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu. Debora ambaye ana uraia pacha wa Congo Brazaville lakini anachezea timu ya taifa ya Gabon anamudu pia kucheza kama kiungo mkabaji ingawa anapendelea zaidi kucheza kama kiungo wa kati (namba 8).

Debora

7. Augustine Okejepha

Klabu ya Simba SC imetangaza kumsajili Augustine Okejepha kutoka Rivers United. Okejepha amesaini mkataba wa miaka 3 na mabingwa wa soka Simba Sc huku ikisemekana atalipwa mshahara wa USD 6000.

Okejepha

8. Valentino Mashaka

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mshambuliaji Valentino Mashaka (20) kutoka Geita Gold .Msimu uliopita alifunga goli 6,Assit 1,mechi 24 sawa na dk 1499.

Valentino

9. Omary Abdallah Omary

Klabu ya Simba SC imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo wa bori, Omary Abdallah, kutoka timu ya Mashujaa FC ya Kigoma. Omary Abdallah, mwenye umri wa miaka 23, ni mchezaji mpya wa tisa kujiunga na kikosi cha Simba SC kuelekea msimu wa 2024/2025. Huu ni usajili wa maana kwa Simba SC, timu ambayo inaendelea kuimarisha safu yake kwa wachezaji wenye vipaji na uwezo mkubwa.

Omary Abdallah Omary

10. Valentin Nouma

Simba SC imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa timu ya taifa ya Burkina Faso na FC Lupopo, Valentin Nouma mwenye umri wa miaka 24 kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Valentin Nouma

11. Karaboue Chamou

Klabu ya Simba SC imethibitisha kuinasa saini ya mlinzi wa kati Karaboue Chamou raia wa Ivory Coast 🇨🇮 kutoka klabu ya Racing Club d’ Abidjan kwa mkataba wa miaka miwili.

Karaboue Chamou

12. Yusuph Kagoma

Klabu ya simba imemtambulisha kiungo Mkabaji Yusuph Kagoma kama mchezaji mpya katika kikosi cha Simba SC kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Singida Fountain Gate. Kwenye NBC Premier League msimu wa 2023/24, Kagoma alicheza mechi 18 akitumia dakika 1373.

Yusuph Kagoma

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Magoli ya Stephan Aziz NBC 2023/2024: Orodha Kamili ya Timu Alizozifunga
  2. Wachezaji walioachwa na Simba 2024/2025
  3. Wachezaji Wanaolipwa Pesa Nyingi Yanga 2024/2025
  4. Simba Imetangaza Kuachana na Shaban Chilunda
  5. Mishahara Ya Wachezaji Wa Simba 2024/2025
  6. Wachezaji Wanaolipwa Pesa Nyingi Simba 2024
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo