Komasava Challenge Yazidi Kushika Kasi: Chris Brown Atoa Video Akicheza
Angalia hapa Video ya Chris Brown Akicheza Challenge ya Komasava inayo trend kwa mitandano Tanzania.
#KomasavaChallenge sio mchezo tena! Wimbo wa Diamond Platnumz, “Komasava,” umevuka mipaka ya Afrika na sasa unatikisa dunia nzima, huku mfalme wa R&B, Chris Brown, akijiunga na katika challenge ya ngoma hio ambayo imekua wimbo wa kimataifa.
Video ya Chris Brown Akicheza Challenge ya Komasava
Video ya Chris Brown akicheza kwa madaha kwenye wimbo wa Komasava imesambaa kama moto sheli kwenye mitandao ya kijamii, hasa TikTok na instagram. Hii sio mara ya kwanza kwa Breezy kuonyesha upendo wake kwa muziki wa Afrika, lakini video hii imeongeza mafuta kwenye moto wa Komasava Challenge na kuibua tofauti kwa wapenzi wa mziki wa Bongo flavour na Bongopiano.
View this post on Instagram
Salmin Maengo, maarufu kama S2Kizzy, ndiye mtayarishaji nyota nyuma ya wimbo huu wa kipekee. Katika mahojiano ya hivi karibuni, S2Kizzy alifichua kuwa “Komasava” ilirekodiwa ndani ya dakika sita tu wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani! Ni wazi kwamba uchawi wa muziki hauhitaji muda mrefu kuundwa.
Mastaa wa Bongo Fleva Watoa Pongezi Kwa Diamond Platnum
Mastaa mbalimbali wa mziki wa Bongo Fleva wametoa pongezi zao kwa Diamond Platnumz na S2Kizzy kwa mafanikio haya makubwa ambayo wengi wameyaita kama mafanikio ya Taifa zima. Jay Melody, D Voice, na Barnaba wote wametoa maoni yao ya pongezi kwenye mitandao ya kijamii, wakishangazwa na jinsi Komasava Challenge inavyopeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
Mapendekezo Ya Mhariri: Orodha ya Wasanii Matajiri Tanzania 2024
Leave a Reply