Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Biashara Ya Duka La Rejareja

Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Biashara Ya Duka La Rejareja 2024: Leseni ya Biashara ni kibali cha kufanyabiashara ambacho hutolewa na mamlaka husika kwa wafanyabiashara au mtoa huduma. Leseni ya Biashara hutolewa kwa mujibu wa sheria ya Leseni ya Biashara Na.25 ya mwaka 1972 na marekebisho yake.

Jinsi Ya Kupata Leseni Ya Biashara Ya Duka La Rejareja

Makundi Ya Leseni Za Biashara

Leseni za biashara zina makundi mawili ambayo ni kundi A na kundi B

1. Leseni Kundi A ni leseni za biashara zenye mtaji mkubwa ambazo hujumuisha leseni za wauzaji wa bidhaa nje ya nchi, huduma za mawasiliano, bandari, vilabu vya usiku, bima, huduma za utalii, benki na taasisi zingine za fedha pamoja na maduka ya kubadilishana fedha, kundi hili la leseni za Biashara hutolewa na Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni ( B RELA )

2. Kundi B ni Leseni za Biashara zinazotolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa anayetoa Leseni za Biashara ni Afisa Biashara wa Halmashauri Katika kundi B kuna biashara za migahawa, hoteli za kawaida, vyama vya ushirika, wakala wa Bima, usajili wa abiria,viwanda vidogo, udalali,utaalam na ushauri, uuzaji wa bidhaa jumla na rejareja.

Mambo Muhimu Yanayotakiwa Kuonekana Katika Leseni Ya Biashara

  1. Namba ya leseni .
  2. Aina ya leseni .
  3. Jina la mamlaka iliyotoa leseni.
  4. Namba ya mlipa kodi ( TIN) .
  5. Jina la kampuni au muombaji wa leseni .
  6. Mahali biashara ilipo .
  7. Kiasi cha ada kilicholipwa .
  8. Namba ya stakabadhi na tarehe ya malipo .
  9. Sahihi ya mtoaji wa leseni .
  10. Jina na muhuri wa mamalaka husika.

Leseni ni kinga ya biashara yako, epuka usumbufu nenda kachukue leseni yako katika mamlaka husika ili ujitendee haki wewe mwenyewe, biashara husika pamoja na wadau unaohusiana nao katika biashara yako .

Vigezo Vya Kupata Leseni Ya Biashara

Muombaji wa Leseni ya Biashara anatakiwa kujaza fomu ya maombi ya Leseni ya Biashara na wakati wa kurejesha fomu muombaji anatakiwa kuambatanisha nyaraka zifuatazo;

  1. Hati ya kujiandikisha kama mlipa kodi ( T IN ) kutoka mamlaka ya mapato Tanzania ( TRA ) .
  2. Cheti cha usajili wa kampuni kama leseni inayoombwa ni ya kampuni.
  3. Mkataba wa pango kama sehemu ya biashara umepanga.
  4. Cheti cha uthibitisho wa mlipa kodi ( T ax Clearance Certificate ) kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ( T RA ) .
  5. Kwa muombaji wa Leseni ya Biashara ya huduma za kitaalamu atatakiwa pia kuambatanisha vyeti kutoka mamlaka husika mfano TCRA (k wa leseni ya huduma ya mawasiliano, TBS ( kwa biashara ya huduma ya chakula ) , EWURA kwa biashara ya uagizaji au usambazaji wa mafuta., TMDA kwa biashara ya dawa.
  6. Pia katika masuala ya sheria, udaktari, uhandisi ni lazima kuambatanisha hati ya kitaalam ( Professional Cerificates ) .

Namna Ya Kufanya Malipo Ya Ada Ya Leseni Ya Biashara

Leseni za Biashara hutolewa kupitia Mfumo wa Mapato ( Local Government Revenue Collection System ) na malipo hufanyika kwa njia ya Mfumo na si kukabidhi fedha kwa mtunza fedha wa Halmashauri kama ilivyokuwa awali.

Mteja anayelipia Ada ya Leseni ya Biashara akiwa na nyaraka zote muhimu ataandaliwa Bill na Afisa Biashara na atawasilisha fedha Benki kiasi kilicho andikwa kwenye Hati ya Malipo na Mtunza fedha wa Halmashauri..

Kiwango Cha Ada Ya Leseni Ya Biashara

Ada ya Leseni ya biashara hulipwa kutokana na aina ya Biashara inayo ombewa Leseni na sio ukubwa wa mtaji pia ada hutofautiana kati ya maeneo ya Halmashauri za Wilaya, Halmashauri za Miji, Halmashauri za Manispaa na Majiji.

Muda Wa Matumizi Ya Leseni

Leseni ya Biashara hutumika kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu tarehe ilipotolewa mpaka ukomo wa matumizi yake .

Faida Ya Kuwa Na Leseni Ya Biashara

  1. Kutambulika kisheria .
  2. Kusaidia wakati wa kufungua akaunti ya Biashara.
  3. Nyaraka inayotumika wakati wa kukopa fedha katika taasisi mbalimbali za fedha.
  4. Kuepuka usumbufu wa kufungiwa Biashara .
  5. Kukuza pato la Taifa .

Masharti Ya Leseni Ya Biashara

  1. Hutaweka masharti yoyote kwa mnunuzi.
  2. Utatoa risiti kwa mauzo yote.
  3. Utafuata sheria ya leseni ya Biashara ya mwaka 1972 na 1980.
  4. Hutauza huduma au bidhaa ambazo hazizingatii viwango vya ubora vilivyowekwa na vyombo vinavyohusika .
  5. Leseni inaweza kunyang’ a nywa wakati wowote ikiwa itaonekana kwamba ulipata kwa udanyanyifu au umekiuka masharti ya Leseni .

Mapendekezo Ya Mhariri:

  1. Jinsi Ya Kuangalia Taarifa Zangu Za NIDA 2024
  2. Jinsi ya Kuangalia Namba ya NIDA Online 2024
  3. Jinsi ya Kujua Kama Namba Ya NIDA Ipo Tayari 2024
  4. Jinsi Ya Kupata Namba Ya NIDA Kwa Simu 2024
  5. Jinsi Ya Kuangalia Deni La Gari 2024 (TMS Traffic Check)
  6. Jinsi ya Kukopa Salio Airtel (Menu Ya Kukopa Salio Airtel)
  7. Jinsi Ya Kuangalia Namba Ya Simu Airtel, Vodacom, TTCL, Tigo & Halotel
Nina uzoefu wa miaka zaidi 6 katika uandishi wa habari nchini Tanzania. Shauku yangu ni kuleta habari muhimu katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu na Michezo